Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma Mh.Atashasta Justus Nditiye amefariki Dunia.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Nditiye amefariki wakati akipatiwa matibabu jijini Dodoma baada ya ajali ya gari aliyopata Februari 10 mwaka huu eneo la Nanenane Nzuguni.
Kutokana na kifo hicho, Spika Ndugai ameahirisha shughuli za Bunge hadi kesho Jumamosi wakati itakapotolewa taarifa na taratibu za kuaga mwili kwaajili ya mazishi.
Atashasta Justus Nditiye alikuwa Mwanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi. Aliwahi kuwa Naibu waziri Ofisi ya Kazi,Uchukuzi na Mawasiliano.
www.simamia.com na Simamia TV inatoa pole kwa wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Familia ya marehemu Nditiye,ndugu jamaa na marafiki wote. Bwana alitoa,Bwana alitwaa na Jina la Bwana lihimidiwe.
Recent Comments