CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuungana kwa vyama vinne ya siasa vya upinzani na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) hasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ni sawa na kujiua kisiasa na kukijenga zaidi Chadema.
Chama hicho kimewataka wafuasi wa vyama vya Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD kuamka kwa kuwa tayari umoja huo umekuwa wa kilaghai na kwamba athari zake zitaonekana baada ya uchaguzi.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Michezo Mjini Nachingwea jana, aliyekuwa mbunge wa Nkenge, Assumpta Mshama, alisema kujiunga kwa vyama hivyo hasa katika uchaguzi kwa kasimamisha mgombea mmoja wa urais na wabunge kumeviua vyama hivyo kisiasa.
âNawaambia hakuna cha Ukawa wala cha upawa, hawa wenzetu wamejiua eti wameungana hivi wanafikiri uchaguzi ukiisha Mbowe (Freeman) atawapatia ruzuku kutokana na kura za Uraisâ Alisema Mshama.
Alisema kwa mujibu wa sheria, chama kinachosimamisha mgombea urais kura zake za urais ndizo zinazokadiria kiwango cha chama husika kupata ruzuku na idadi ya wabunge wa viti maalumu.
âSasa hebu niambieni nyie CUF mmemsimamisha nani kugombea Urais? Mnadhani Mbowe ninayemjua mie atawagawia ruzuku? Au kuchagua viti maalum kwa usawa, mmeshajiua kisiasa,â alisisitiza.
Alisema hata wabunge wa viti maalumu wakichaguliwa kupitia Ukawa, lazima wajiunge kwanza na Chadema.
âSasa nyie wenzangu na mie mmekaa hapa mnajisifu na kupigia debe Ukawa kwa lipi?â Alihoji. âNawashangaa mnavyopigia debe Ukawa, mnaipigia debe Chadema. CUF, NCCR na NLD mmeshafutika, hamna lenu tena,â alisisitiza.
Naye aliyekuwa Katibu wa Uenezi Taifa wa Chadema, Greyson Nyakarungu, alisema anavishangaa vyama hivyo vya CUF, NCCR na NLD vinavyompigia debe mgombea Urais wa Chadema, Lowassa.
âNawasikitikia kwa kumpigia debe Lowassa nawaambia mnajidanganya, huu Ukawa umeanzishwa kwa ajili ya kuua vyama vya upinzani na kukijenga Chadema,â alisema Nyakarungu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi (CCM), Ally Mtopa alisema tayari katika mkoa huo wapinzani na hasa CUF `wameshakufaâ na sasa wamebaki kugombana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ruangwa, Fadhil Liwaka, alisema CUF ilishakufa kwa kuwa kitendo cha kuchukuliwa kwa Duni aliyekuwa Makamu wa Chama hicho na kuingia Chadema, kimekimaliza kabisa chama hicho.
âNawaambia ukweli hata leo hii Chadema ishinde au isishinde vitim aalum CUF na vyama vingine haiwezekani mpaka wagombea wao wajiunge Chadema, sasa hapo kuna CUF kweli?â Alihoji Liwaka.
Recent Comments