Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony Mavunde leo ameandika historia mpya kwenye maisha ya wananchi wa Mtaa wa Mayeto Hombolo Makulu kwa kusaidia uchimbaji wa kisima cha maji kupitia Taasisi ya ISLAMIC HELP na hivyo kupunguza adha ya wananchi hao kutembea zaidi ya Kilomita 4 kufuata maji.
Kisima hicho kitahudumia zaidi ya wananchi 8000 wa Mtaa huo wa Mayeto na kuwaondolea adha ya kwenda umbali mrefu ambapo baadhi ya wakinababa wamesema sasa watakuwa na amani kwa kuwa muda ambao wakina mama wanafuata maji ni mrefu sana kiasi kwamba kuwapelekea kufikiria mambo tofauti zaidi ya kuchota maji. “Niliahidi kujenga Shule ya Msingi na kuchimba kisima,leo nasimama hapa kwa furaha kubwa kwa kuwa ninyi ni mashahidi kwamba ujenzi wa Shule unaendelea na leo maji yamepatikana.
Maji haya yatasaidia kuwaondolea adha wananchi wa hapa Mayeto ya kutembea umbali mrefu kwa kuwa sasa hivi mtayapaata mita chache kutoka katika makazi yenu,maji haya yawe chachu ya maendeleo katika eneo letu ili kupitia huduma hii tuboreshe Afya na ustawi wa wananchi”Alisema Mavunde
Akizungumza kwa niaba ya Wananchi,Mwenyekiti wa CCM Kata ya Hombolo Makulu Ndg. Vicent Mtwangulu amemshukuru sana Mbunge Mavunde kwa namna alivyosaidia katika utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi wa kata hiyo na kuwataka kumuombea kwa Mungu ili aendelee kuigusa jamii ya Wanadodoma kupitia uongozi wake.
Recent Comments