Mzee Ntukamazina ni Mfano wa Kuigwa. Ndivyo baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Ngara wanavyosema pale wanapomtaja Mzee Deogratius Ntukamazina aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara 2010-2015.
Kupitia kundi la Whatsapp linalowashirikika wananchi wanaotoka wilaya ya Ngara,ambao wanaishi sehemu mbali mbali Duniani wanajadili masuala ya maendeleo ya Jimbo la Ngara hasa wakati huu ambapo Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi mkuu Oktoba 2020.
Moja ya mijadala inayoendelea ni juu ya maendeleo yaliyofikiwa baada ya muhula wake wa utawala, ambapo aliyechukua kijiti kupitia Uchaguzi wa 2015 ni Bw.Alex Gashaza ambaye anahitimisha mhula wake wa Uongozi. Mijadala hiyo inahusu pia ripoti ya maendeleo jimboni.
Mmoja wa wanakundi ni pamoja na Mzee Deogratius Ntukamaziana, ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Ngara kwa mhula mmoja kuanzia 2010 hadi 2015.
Ifuatayo ni sehemu ya mchango unaozungumzia mafanikio,na repoti ya utendaji wakati wa Uongozi wake:-
Salaam wana Jamvi la Umoja wa Wana Ngara, kwanza niwapongeze kwa jinsi mlivyo na Uzalendo kwa Wilaya yenu ya Ngara. Hongera sana. Uzalendo huo unadhihilishwa na hoja mnazozitoa hapa kwenye Jamvi. Mimi na labda Wazee wengine nimeamua kuwa a “Silent observer’ ili kuwaacha Vijana wajifunze namna ya kujenga hoja lakini wakiwa makini na source of Information kwa maana usipokuwa na uhakika juu ya chanzo cha habari fulani you have no right to speak.
Katika hii debate kuhusu Riport ya Mbunge Gashaza kuna jamaa mmoja amesema hajui barabara ya Rulenge ya Ntukamazina inaanzia wapi na inaishia wapi labda ni ya kukinga vumbi kwenye nyumba yake ya Munjebwe. Jambo hilo limenisukuma niweke kwenye Jamvi ukweli wa mambo.
- Hakuna barabara ya Ntukamazina. Nilipokuwa Mbunge niliiomba TAMISEMI Idara ya Engineering waweke Lami nyepesi katika barabara za mjini Ngara na kweli Mwaka 2015 wakati namalizia kipindi changu cha Ubunge walianza kuweka lami nyepesi katika barabara za mjini Ngara. Sikuiomba Tamisemi iweke lami nyepesi katika mitaa ya mji wa Rulenge badala yake nilimuomba Regional Manager wa TANROADS wa Kagera aweke lami nyepesi kuanzia Mission ya Runge kuelekea Ngara ili kupunguza vumbi kwenye mji wa Rulenge.
- Wakati naomba lami nyepesi kwa Mji wa Ngara na Rulenge nilishaiomba Benki ya Afrika watujengee Barabara ya Nyakahura–Kumubuga–Keza–Rulege–Murugarama kwa kiwango cha lami. Huo ulikuwa mwaka 2011. Mwaka huo nilikutana na rafiki yangu Dr. Donald Kaberuka Rais wa Benki ya Afrika (AfDB) Arsha. Rais huyo alikuwa Mnyarwanda ambaye aliniheshimu kama Kaka yake. Alikulia Karagwe Tanzania na alisoma Degree ya kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Nilipokutana naye 2011 mjini Arusha nilimuomba mambo mawili (i). Barabara hiyo niliyoitaja (ii). Kuboresha Mabonde yote ya Wilaya ya Ngara kwa ajili kilimo cha mpunga na mazao mengine. Alinikubalia maombi yote mawili na akaniambia niiombe Serikali ipeleke AfDB Maombi rasmi.
Kazi hiyo niliifanya kwa kuwaomba Mawaziri wa Ujenzi na Kilimo–Mh Waziri Magufuli wa Ujenzi na Waziri wa Kilimo Mh Christopher Chiza. Bahati nzuri Mh Magufuli alifanya haraka kutuma Ombi la serikali na Bodi ya AfDB ikaidhinisha Mkopo kwa ajili ya Barabara ya Nyakahura–Rulenge– Murugarama.
Bahati mbaya Mh Chiza Waziri wa Kilimo alichelewa kupeleka Ombi la Serikali kuhusu Uboreshaji wa Mabonde na ilipofika 2015 rafiki yangu Dr Donald Kaberuka alimaliza muda wake wa Urais wa AfDB.
Rais Magufuli anajua kwamba fedha hizo zipo ila wamechelewesha Upembuzi yakinifu. Nilimkasrikia sana Waziri Christopher Chiza. Baada ya mimi kustaafu nilimuomba Eng Deusdedit Kakoko afanye ufuatiliaji wa barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha lami. Eng Deus anafanya hiyo kazi.
- Mimi ndiye nilileta Baraza la Ardhi Ngara. Wazee wenye kesi za Aridhibwalikuwa wanahangaika kwendà Chato kwenye Baraza la Aridhi.
- Nilileta Maktaba 2 za Ngara na Rulenge kwa kumuomba
Mkurugenzi wa Maktaba Kuu ya Taifa Dr Mcharazo.
- Niliwaomba DGs wa TASAF na MKURABITA waleta Mipango hiyo Wilayani Ngara.
Katika Mkoa wa Kagera Ngara ilikuwa ya kwanza kupokea Mradi TASAF–Mpango wa kusaidia kuinua hali za Kaya Maskini sana. Ngara pia ilikuwa Wilaya ya kwanza kuletewa MKURABITA– Mpango wa kurasimisha mali na Biashara za Wanyonge.
Tulianza na Vijiji vya Buhororo na Munjebwe. Niliweza kufanya hivyo kwa sababu nilikuwa Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ambayo ilikuwa inasimamia Miradi hiyo miwili.
- Nilianzisha VICOBA katika Kata zote 22 na nikamuomba Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Bwana Sabasaba kutoa Mikopo isiyo na riba kwa VICOBA.
Mkurugenzi Mkuu Sabasaba alituma wataalamu wake Ngara lakini bahati mbaya nikawa nimestaafu sidhani kama Benki hiyo ya Posta ilitoa mikopo.
- Nilianzisha Mfuko wa Elimu kwa kila Kata lakini nasikia Mifuko hiyo haikuendelezwa
- Niliiomba Serikali ipandishe hadhi mji wa Rulenge kuwa Mamlaka ya Mji mdogo na Serikali ilikubali ombi langu. Kwa hiyo Wilaya ya Ngara ina Mamlaka mbili za Miji midogo– Ngara na Rulenge.
Nilimuomba Waziri wa Afya aidhinishe Nyamiyaga kuwa Hospitali kamili na ombi langu lilikubaliwa lakini Murgwanza iliendelea kuwa Hospitali Teule ya Wilaya. Kwa kutumia Ubunge wangu na Uwenyekiti wangu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nilihakikisha Hospitali ya Murgwanza inapata Mkopo wa Bima ya Afya wa Sh Millioni 42 wakajenga Duka la dawa.
Hospitali ya Rulenge ilipewa mkopo wa Shilingi Milloni 40 kwa ajili ya ukarabati na ununuzi wa Vifaa tiba. Hospitali ya Nyamiyaga ilipewa Mkopo wa Shilingi  Million 20 walinunua mashine ya Ultra Sound. Pia nilihakisha kila hospitali inapewa Mashuka 100 na Mashuka 20 kwa kila Kituo cha Afya– Mabawe, Lukole, Bukiriro na Murusagamba.
- Nilihakikisha Ngara inakua miongoni mwa Wilaya chache za kupewa Ruzuku ya pembejeo.
- Nilisambaza Vitabu katika Shule mbali mbali za Msingi na Sekondari kwa kutumia Basi la TAQWA linalokwenda Burundi kuvitoa DSM hadi Ngara na kuwaomba Ma DEOs wa Primary na Sekondari kuvisambaza.
11 kwa kutumia Mfuko wa Jimbo tulijenga Visima vya Maji kwenye Shule za Sekondari Kanazi, Muruvyagira, Ndomba na Nyakisasa.
- Nilichangia ujenzi wa Vituo vya Polisi Muruvyagira, Djululigwa, Keza na Murubanga.
- Niliibana REA Ikawasha Umeme Mugoma, Rusumo, Benaco, Muruvyagira na Rulenge kabla ya kustaafu. Niliiomba REA kujenga Substation ya Djululigwa ili kuboost umeme wa Rulenge na Vjiji vya jirani na Djululigwa.
- Nilifuatilia Mradi wa Maji wa Benki ya Dunia katika Vijiji 10. Wakati nastaafu Vijiji vya Ngundusi, Rulenge na Munjebwe vilikuwa vimepata maji ya bomba.
- Niliibana Serikal na Ubalozi wa Holland kukamilisha Umeme wa Orio Holland kwa kuweka Generata 2 kubwa pale Tanesco Ngara kwa ajili ya line ya K 9– Kasharazi-Mikole–Nyamahwa– Nyankende, Kashinga mpaka Rulenge Sekondari.
Naomba kwa leo niishie hapa nitaendelea hapo baadae.
RIPOTI YANGU YA MAMBO NILIYOYAFANYA NA VIPORO VYAKE NILIMKABIDHI NDUNGU ALEX GASHAZA 2015 kwa kuendeleza nilipoishia.
Tangu Uhuru nilikuwa Mbunge wa kwanza KUKABIDHI KIJITI KWA MBUNGE MPYA KWA MAANA NILIKUWA NIMEJIANDAA KUSTAAFU. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa FURSA YA KUWA MCHUNGAJI MWEMA WA KONDOO WAKE WA NGARA kwa Miaka mitano.Haya niliyoweka hapa Jamvini ni sahihi kwa 100%.
Mzee Deogratias Aloys Ntukamazina
Recent Comments