NA,ANKO G
Katika eneo la Kabanga Makao makuu ya kata (Kabanga Mjini)wilayani Ngara mkoani Kagera baadhi ya mitaro iko hatarini kutoweka baada ya kujaa udongo/mchanga unao tokana na nmomonyoko wa udongo.
Vilevile simamia.com imepita katika baadhi ya maeneo na kushuhudia baadhi ya karavati zikiwa zimejaa udongo kiasi cha kushindwa kupitisha maji ipaswavyo.
Pia kuziba kwa mitaro hii inaweza kupelekea kutokea kwa mafuriko hasa katika kipindi hiki cha masika na hata kupelekea kuharibu kingo za barabara.
Hivyo basi simamia.com inashauri siku ya alhamisi ambayo ni siku maalumu kwaajili ya usafi wilaya ya Ngara ni vyema kutumia siku hiyo kusafisha mitaro hiyo.
Ikumbukwe kuwa mitaro imewekwa kwa kusudi la kupitisha maji hasa kipindi cha mvua lakini mitaro hiyo inaziba kutokana na mmomonyoko wa udongo unaotokana na shughuli za kibinadamu za kila siku hivyo ni mhimu kufanya usafi katika mitaro hiyo marakwamara.
Recent Comments