NA,ANKO G
Mkuruge mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Ngara Simon Thobias Mtuka ametoa siku kumi na nne (14) kwa Anania Jonathan mkazi wa Kitongoji cha Kabulanzwili, Kijiji cha Kasharazi na kata ya Rusumo Wilayani Ngara Mkoani Kagera kusitisha ujenzi na kubmoa majengo mawili kwa kinacho dawaiwa kuwa amekiuka utaratibu na kanuni za ujenzi.
Aidha Jonathan aliandikiwa barua hiyo tarehe 04/11/2024 baada ya utafiti na ukaguzi uliofanywa na timu ya wakuu wa idara ya Aridhi kitengo cha Mazingira na idara ya maendeleo Vijijini na Mijini kutoka Wilayani Ngara ulio fanyika tarehe 01/11/2024.
Aidha barua hiyo imeanisha vifungu vya sheria vinavyo mtaka bwana Jonathan kusitisha na kubomoa majengo hayo kama inavyo onekana.
Pia Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Ngara Philimon Charles Kanwakabo ameiambia simamia.com kuwa suala hilo ni la kisiasa kwasababu zuia hilo limefanyika baada ya Anania Jonathan kuonekana anagombea uenyekiti kwasababu amekua akiishi katika nyumba mojawapo kwa muda usiopungua miaka 8 mpaka linapokuja zuio hilo.
Mwenyekiti huyo ameongeza na kusema kuwa wakati Anania Jonathan akiwa chama cha Mapinduzi (CCM) hakusumbuliwa juu ya majengo hayo hivyo zuio hilo linatokana na Mgombea huyo kuhamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivyo analichukulia zoezi hilo kuwa ni shinikozo la kisiasa.
Lakini pia Mwenyekiti huyo amemaliza kwa kusema kuwa alimtafuta Mkurugezi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Ngara na kumuahidi kuwa atalimaliza lakini mpaka sasa bado hapewi majibu ya kuridhisha.
Recent Comments