MWANAFUNZI wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mwagiligili, iliyopo Misungwi, mkoani Mwanza, Rahel Emmanuel (13), amekutwa amekufa baada ya kujinyonga ndani ya nyumba ya Mwalimu wake Mkuu, John Msusa.
Akizungumzia tukio hilo, Mwalimu Msusa alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa sita mchana.
Alisema kabla ya kifo hicho, mwanafunzi huyo ambaye ni mtoto wa shemeji yake, aliyeanza kuishi naye tangu akiwa mdogo alikutwa na karatasi katika madaftari yake iliyokuwa na maneno ya mapenzi na alihojiwa ofisini na kuruhusiwa kwenda nyumbani kumpikia mtoto chakula, ndipo akajinyonga.
âHuyu mwanafunzi alikamatwa na kipande cha karatasi katika madaftari yake kilichokuwa na maneno ya mapenzi, tulimhoji ofisini na kumruhusu kwenda nyumbani kumpikia uji mtoto aliyekuwa analia, sasa alipofika nyumbani kwangu alifanya uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kamba ndani ya nyumba tunayoishi.
âHatujui alifikiria nini hadi kuchukua uamuzi wa namna hiyo, hili suala tunawaachia vyombo vya dola ili kuchunguza zaidi,â alisema Msusa.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwagiligili, Herman Paulo, alikiri kutokea tukio hilo na alisema alichukua uamuzi wa kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Misasi na walifika na kufanya uchunguzi na kuruhusu mwanafunzi huyo kuzikwa jana katika Kijiji cha Kanyerere.
Pia Ofisa Elimu ya Msingi Wilaya ya Misungwi, Efram Maginge, alisema wamepata taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo, aliyekuwa miongoni mwa waliotarajiwa kuhitimu mwaka huu.
Polisi wilayani Misungwi nao wamethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na walisema hakuna wanayemshikilia.
Recent Comments