NA
ANKO G
Soko la Mkavumu ni soko linalopatikana katika kitongoji cha Mndimanga kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera ni soko linalo kusanya wakazi wa kata ya kabanga kia siku ya jumapili ambapo bidhaa mbalimbali huuzwa katika soko hili.Aidha soko hili linafahamika kama Garama ndaje (Kihangaza) neno linalo tafsiika kama Lala chali nakuja ambapo ni kama jina la utani na jina hilo linaonekana kupoteza mvuto kutokana na watu kuto litaja na watumiaji wa soko hilo kuonekana kutovutiwa nalo.
Vilevie neno Mkavumu (Kihangaza) linatafsiriwa kama Mrumba ikiashiria miti ya jamii ya mirumba inayo onekana kushamiri katika soko hili ambayo husaidia kuleta kivuli kipindi cha kiangazi na jua kali lakini miti hiyo huleta kero kipindi cha mvua maana mvua inapo maliza kunyesha basi miti hiyo hubaki na majimaji ambayo huanza kudondoka na kuwadondokea watumiaji wa soko hilo.
Hata hivyo soko hii hutumika siku ya jumapili ambapo siku za tofauti soko hili huwa na muonekano huu ambapo ni vibanda ambavyo vimejengwa kwa miti lakini ikifika siku ya jumapili vibanda hivyo huwekewa turubai kwaajili ya kuzuia mvua na jua huku wengina wakipanga bidhaa zao chini bila kuweka vibanda wala turubai.Lakini pia bidhaa zinazo uzwa katika soko hili ni pamoja na Nyama ya Nguruwe (Kitimoto) ambapo wauzaji hutumia meza kama hii kuwekea nyuma huku eneo jingine likitumika kukatia nyama na kuchoma kwa wale wateja wanao tumia nyama zilizo chomwa ama kukaangwa.
Pia Nyama ya Nguruwe maranyingi hundana na pombe ambapo katika soko hili huuzwa pombe mbalimbali kama vile pombe za viwandani pamoja na pombe za kienyeji Gwagwa (Rubisi), Gongo, Mgorigori, Mnanasi n.k (Kihangaza) na watumiaji wa soko hili ambao ni watumiaji wa pombe hizo hukaa katika mabenchi haya wakati wakipata vinywaji hapo.
- Waswahili husema Nyumba ni choo hivyo katika soko hili halijakosa choo huu ndio muonekano wa choo ambacho kinatumiwa na watumiaji wa soko hili na ni choo chenye matunndu mawili choo chakike na cha kiume lakini ni hatarishi kwa afya za wtumiaji wa soko hili hususa ni kipindi cha mvua wanakua hatarini kupatwa na magonjwa ya mripuko ambapo baadhi yao hujisaidia katika vichaka vilivyopo jirani na soko hilo pamoja na makazi ya watu kwa kuhofia magonjwa.
Recent Comments