Recent Comments

MUONEKANO WASASA WA MAEGESHO YA MAROLI NZAZA NA SOKO LA KIMKAKATI

By Simamia Ngara Jul 9, 2024
Exif_JPEG_420

NA,ANKO G

Eneo la soko la kimkakati lililopo kitongoji cha Nzaza ‘A’ Kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera limewahi kutumiwa kama eneo la magesho ya magari ya mizigo ambapo baadae mkuu wa mkoa Fatma Mwasa alitoa maelekezo maegesho hayo yarudi katika eneo la zamani na endepo magari yakijaa maegesho ya zamani basi mengine yaegeshwe katika eneo hilo la soko wakati mchakato wa ujenzi wa soko hilo la kimkakati ukiendelea.

Aidha katika siku ya leo camera ya simamia.com imemulika katika eneo hilo na kushuhudia idadi ya magari yaliyo egeshwa katika eneo hilo yakiwa machache ukilinganisha na maegesho halisi.

MAGARI yakisubiri kuvuka kuelekea Burundi

Hata hivyo eneo hilo kwasasa linatumika kama kituo cha kupakia matunda aina ya Parachicho na Ndizi wakati wa kusafirisha matunda hayo kupelekea mikoa mbalimbali.

Hata hivyo wananchi wa Kabanga na nchi jirani ya Burundi wanasubilia kwa hamu ujenzi wa soko hilo la kimkakati ambalo limekua ahadi kwa muda mrefu bila mafanikio.

Vilevile camera za simamia.com imemulika katika lango la kuingilia katika eneo hilo na kushuhudia likifanyiwa ukarabati ili kuboresha eneo hilo kuweza kuhimili uzito wa magari yanayo ingia na kutoka katika.