SALVATORY NTANDU
SHINYANGA
14/2/2021
Mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha kwa muda wa dakika 45 katika mkoa wa Shinyanga imezua taharuki baada ya kukata mawasiliano ya barabara ya kwa zaidi ya saa 5 katika barabara ya Ibinzamata kuelekea kata ya kitangiri baada ya maji kuziba daraja na kupita juu na kuzuia watu na magari kupita.
Mvua hiyo imenyesha jana majira ya mchana imeharibu miundombinu ya barabara,kuangusha miti pamoja na mazao ya wananchi sambamba na kuzuia shughuli za uzalishaji mali kutokana na kuziba kwa daraja hilo ambalo ni kiunganishi kikuu kati ya wakazi wa kata za Ibinzamata na kitangiri.
Wakizungumza na Simamia blog baadhi ya wananchi waliopata athari za mvua hiyo Mwasiti Shabani mfanyabiashara wa nyanya katika soko la kitangiri alisema kuwa mvua hiyo imesababisha yeye kupata hasara ya zaidi ya shilingi laki mbili baada ya nyanya zake kuharibiwa na mvua hiyo yam awe iliyoambatana na upepo mkali.
âNimepata hasara kubwa nyanya zimetobole na mawe ya mvua halafu zingine zimesombwa na maji katika harakati za kuokoa zingine zisisombwe na maji,tunaiomba serikali ituboreshee mazingira ya kufanyia biashara sisi wajasiriamali wadogo,âalisema Shabani.
Hamduni Jumanne ni mmoja ya wakazi wa kitangiri alisema endapo serikali ikijenga daraja kubwa katika eneo hilo wakazi wa maeneo hayo hawatakubwa na mafuriko ya mara kwa mara kama inavyotokea pindi mvua kubwa inaponyesha kila mwaka.
âKila mwaka tunapata mafuriko katika eneo hili,daraja lilipo ni dogo maji ya kizidi linaziba na kusababisha maji kwenda kwenye makazi ya watu,ikiwemo katika soko letu,tunaziomba mamlaka zitusaidie kero hii ambayo imeanza kuleta madhara kwa wananchi hususani watumiaji wa barabara hii,âalisema Jumanne.
Daudi Izengo ni mkazi wa Ibinzamata alisema kuwa serikali inapawa kuliangalia kwa kina daraja hilo ambalo limekuwa kero kwao kwa muda mrefu hali ambayo inaweza kusababisha maafa pindi mvua kubwa zinaponyesha hususani nyakati za usiku ambapo watu wamelala kwa kukumbwa na mafuriko.
Gazeti la Uhuru limefanikiwa kuzungumza na Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga David Nkulila alikiri kuwa na taarifa za kero ya daraja hilo na kusema kuwa watahakikisha wanalipatia ufumbuzi wa haraka ili lisiendee kuzuia shughuli za maendeleo kwa wananchi wa kata hizo.
âMvua kubwa imenyesha na imeleta uharibifu wa miundombinu katika manispaa yetu,niwahakikishie wananchi wasiwe na wasiwasi serikali imeshaanza kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha miundombinu iliyoharibiwa na mvua hiyo inarudi katika hali yake ya kawaida,âalisema Nkulila.
Mwisho.
Recent Comments