Recent Comments

MWANAUME AJICHONGEA JENEZA

By Simamia Journal May 31, 2020

BUKOMBE

Mwanaume mmoja mkazi wa Ushirombo wilayani Bukombe mkoa wa Geita anaishi na jeneza ndani ya nyumba ambalo ameliandaa kwaajili ya mazishi yake pale atakapofariki kutokana na kile anachoeleza kuwa ni kuchoshwa na unyanyasaji wa familia

 

Bw.Sylvester Mihayo ameiambia www.simamia.com kuwa kwa takribani miaka 3  sasa, anaishi bila furaha kutokana na unyanyasaji ikiwa ni pamoja na kipigo kutoka kwa mke wake na watoto hali iliyompelekea kuitelekeza nyumba na kuishi kwenye karakana ya ufundi

 

Amekitaja chanzo cha mateso yake kuwa ni baada ya kuugua kwa muda mrefu  tangu mwaka 2018 ambapo familia ilimtenga na kumzuia kuingia kwenye nyumba yake

“Kweli naishi kwa mateso makali. Nimeugua nimetegwa na familia yangu hata nyumba nimeikimbia kwa sasa naishi hapa kwenye ofisi yangu”

Hata hivyo, mke wake Bi. Vumilia John amekanusha madai yam me wake kunyanyasika na kupigwa kwa madai kuwa yeye na watoto wake waliamua kumtenga kutokana na tabia za ulevi

 

Akizungumzia hali hiyo,Mkuu wa wilaya ya Bukombe  Bw. Said Nkumba amesema hajapata taarifa za Bw. Mihayo na kuahidi kumtafuta ili kupata maelezo ya kina kwaajili ya ufumbuzi.                                    mwisho

 

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv