MA M L A K A ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wakazi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kulipa kodi zao za majengo kabla ya Juni 30, mwaka huu.
Hayo yamesemwa jana jijini hapa na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere wakati alipotoa maelezo ya majukumu ambayo mamlaka yake imepewa ya kukusanya kodi ya majengo kuanzia Julai mwaka jana, kwa viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Mwanza.
Alisema wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana) na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao ili kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili na kulipia kupitia benki yoyote ya biashara.
Alisema TRA Mkoa wa Mwanza inasimamia kodi hiyo kwenye majengo yaliyokamilika au yanayotumika kwa makazi au biashara, yaliyopo kwenye maeneo yaliyopimwa au ambayo hayakupimwa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
Alisema watu wanaoishi kwenye maeneo ambayo nyumba zao zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya jengo kama inavyooneshwa kwenye ankara zao na walioko kwenye maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminiwa watalipa viwango maalumu vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na TRA kwenye vyombo vya habari hivi karibuni. âKwa Jiji la Mwanza watalipa Sh 20,000 na Manispaa ya Ilemela watalipa Sh 15,000 kwa mwaka,â alisema.
Recent Comments