Katika mkutano mkuu uliofanyika Agosti 13, viongozi hao walikiri kuitisha mkutano na waandishi wa habari Agosti 9 bila ya kupata idhini.
Hatua hiyo ilisababisha kujengeka kwa taswira mbaya kiuwajibikaji, kanuni na utaratibu.
Katika taarifa ya Mwenyekiti Maalum wa TEF, Walace Mauggo imeeleza kuwa jukwaa kwa kauli moja limetoa onyo kwa viongozi wake kutorudia yale ambayo yamejitokeza.
âBaada ya kutafakari na kutathmini mwenendo wa mkutano huo, jukwaa lilobaini kuwepo kwa kasoro kubwa wakati wa kurejesha mahusiano wa kikazi na kiongozi ambaye habari zake zilizuiwa kuripotiwa kwa takribani miezi mitano,â imeeleza taarifa hiyo.
Pia wametakiwa kuhakikisha kunapotokea masuala makubwa kama hayo ambayo yashafanyiwa maamuzi na mkutano mkuu na taasisi nyingine za habari yanarudiswa maamuzi kwa wanachama kabla ya hatua za  mwisho.
Mauggo ameeleza kuwa TEF haitasita kuchukua hatua kwa kiongozi au mtu yoyote atakayeonekana kutishia usalama wa wanahabari, uhuru wa uhariri na vyombo vya habari.
Recent Comments