NA,ANKO G.
Mzee Philomon Mihwabale ni mkazi wa Kijiji cha Murukukumbo Kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera anae kadiriwa kuwa na umri kati ya Miaka 80 mpaka 90 ni mzee ambaye alitelekezwa na mke wake kutokana na hali yake ya kiuchumi na kuachiwa watoto wadogo.
Katika mahojiano yake na simamia.com mzee Mihwabale anasema kuwa katika ujana wake amewahi kuoa mke lakini alifariki Dunia ndipo baadae aliamua tengeneza familia nyingine kwakuoa mke wapili ambapo alifanikiwa kuzaa nae watoto wawili wakiume ambapo mwanamke huyo alimtoroka mzee huyo na kumwachia watoto wachanga miaka kadhaa iliyopita ambapo kwasasa watoto hao wanakadiriwa kuwa kati ya Miaka 8 mpaka 10.
Aidha mzee Mihwabale ameieleza simamia.com kuwa watoto hao hawajapata haki yao yamsingi ya kupata Elimu kutokana na yeye kushindwa kumudu gharama na mahitaji yao ya shule licha ya kuwa yeye anatamani watoto hao wasome.
Vilevile mzee Mihwabale hana uwezo wa kufanya kazi yoyote zaidi anategemea watoto hao wamsaidie kazi wakati mwingine akitegemea misaada kutoka kwa wasamalia wema wanao mzunguka.
Pia mzee huyo ameieleza simamia.com kuwa siku kadhaa zilizopita kipindi cha mvua kali alinusurika kuangukiwa na nyumba ambapo majirani wamelazimika kumjengea kajumba ambako anaishi kwasasa katope.
Mzee Mihwabale amemalizia kwa kuwaomba wasamalia wema kumsaidia wanacho jaliwa lakini zaidi akisisitiza kuomba msaada wa watoto wake kusoma.
Kwa upande wa Niyo Philimon Mihwabale na James Philimon Mihwabale ni watoto walio telekezwa na mama yao, wao ombi lao kubwa wameomba wasamalia wema watakao guswa wawasomeshe na kwa ambae ataguswa awasiline na Simamia Media kwa namba +255 748 632 022.
Vilevile Editha Lenard na Olestina Medan ni majirani ambao wamethibitisha kufahamu hali ya mzee huyo na wamekua wakimsaidia vitu mbalimbali ikiwemo chakula, mavazi na Matibabu pamoja na nyumba anayo anaishi kwasasa mara baada ya iliyokuwepo kuanguka lakini wameonesha hali ya kuzidiwa kwakua na wao wana familia zao hivyo wameomba wasamaliawema watakao guswa kumsaidia mzee huyo.
Recent Comments