Recent Comments

Ngara: CCM Tubadili Njia Ndio Tuthaminike?

By Baraka Bitariho Mar 11, 2024
Anayeishi kwenye nyumba kama hii ni mwana Ngara. Mchana anashinda akitafuta kuni na akisikia mlio wa gari anakimbilia gari kumsalimia yule anayemuita Mheshimiwa. Pengine angeitwa Mleta Umasikini kwani anayeishi humu huchagua chama ambacho kimesahau kuleta maendeleo kijijini. Je hata kama aishie humu angepewa uteuzi, angekuwa kilanja bora wa mwenye nazo ama angekumbuka kijijini na kutokomeza umasikini usiofichika huko anapotoka? Pengine ataishi mjini, mbali na waliomchagua na ataogopa kurudi nyumbani kwani hana cha kuonyesha zaidi ya pambio na ahadi hewa wale waliomchagua.
Katika ukurasa wetu wa Tochu Kwa Jamii, andiko lifatalo limeandikwa
Na Sam Ruhuza
*Ndugu zangu Wanangara!*
Nimetafakari sana hizi teuzi serikalini, kuna sehemu sizielewi, mnisaidie!
Ngara kuna watu ccm kwelikweli na vijana wengi wasomi tu, lakini kwenye teuzi, hauwaoni, lakini wanavyojifanya ni ccm damdam hadi unashangaa vipi hawaonekani, lakini maeneo ya wapinzani ndipo teuzi kila kukicha!!
Kigoma walipoamua kura zao kuwapa wapinzani hasa NCCR- Mageuzi majimbo yote, ccm wakashtuka, kila kitu wamepeleka kigoma! Mlezi wa Mkoa ni waziri mkuu, Makamu wa Rais, Waziri, wakuu wa Mikoa, Gavana Benki Kuu, yaani hauwezi kukuta teuzi yoyote hakuna mtu wa Kigoma, Barabara, Maji, umeme na bado kwenye uchaguzi ccm hawana uhakika wa kura za kigoma!
Angalia Kilimanjaro, Arusha na Mara walipoamua kuwapa Chadema! Teuzi na miradi kibao ni maeneo hayo!
Tuje kwenye ziara za viongozi wa serikali, hayo maeneo kila siku wanapishana, lakini Ngara walipoamua wenyewe kuipenda ccm, aibu hata kusema!!
Yaani kuna wakati naona wanangara wanajipendekeza ccm wakati yenyewe hata haiwapendi na ukijifanya kutambua haki yako, wanakuita Mrundi, Mnyarwanda kukukata spidi!!
Kijiji Kiongozi anapotokea kunaweza kuwa na madini mbali mbali ila anayenufaika ni mwenye pesa anayeishi mjini. Huyu anayeitwa kiongozi anajikuta ni kilanja wa vilivyopo na kuangalia pembeni na si kutatua changamoto zilizopo kijijini kwake. Pengine ni chama kinachowapa ridhaa ya uongozi hawa wanaoitwa waheshimiwa na sio kufanya marekebisho kwenye safu ya ukilanja ili wengi waliopo kijijini alipotoka waishi maisha bora.
Angalia hata teuzi za Mbunge wa Ngara, katika historia Ngara hatujawahi kuwa na Waziri kamili, tumeishia kwa Naibu Waziri Afya Mh Sebabii Gwassa 1975 tena nafikiri miaka miwili sikumbuki vizuri na Naibu Waziri Ujenzi na Mawasiliano Mh Gachocha 1985-90 kama sikosei na hao wote ni teuzi za kipindi chao cha kwanza cha uchaguzi, lakini kuanzia hapo hakuna teuzi tena Naibu wala Waziri!
Tumekuwa na Wabunge wasomi kwelikweli, wazoefu wakubwa Serikalini, lakini teuzi hakuna!!
Yaani Ngara ni sahihi sana kusema watu wanajipendekeza ccm wakati wenye chama chao hawawapendi!!
Nimeamua kuandika hili humu, japo wengine watalichukua kisiasa na kuwa na maono tofauti na mengine wanajua wao, lakini naangalia zaidi Maslahi ya Ngara na sitoshangaa baada ya andiko hili, ukaanza kuona teuzi zijazo mtu wa Ngara yumo kwasababu natambua nguvu ya maandiko yangu!
Binafsi Sihitaji uteuzi wowote ule, ila Ngara ni walipa kodi kama wananchi wengine, nitafurahi sana kuona jina la Mwananchi wa Ngara akipata uteuzi wowote angalau ashiriki kwenye kamati za maamuzi!
Anayeishi kwenye nyumba kama hii ni mwana Ngara. Mchana anashinda akitafuta kuni na akisikia mlio wa gari anakimbilia gari kumsalimia yule anayemuita Mheshimiwa. Pengine angeitwa Mleta Umasikini kwani anayeishi humu huchagua chama ambacho kimesahau kuleta maendeleo kijijini. Je hata kama aishie humu angepewa uteuzi, angekuwa kilanja bora wa mwenye nazo ama angekumbuka kijijini na kutokomeza umasikini usiofichika huko anapotoka? Pengine ataishi mjini, mbali na waliomchagua na ataogopa kurudi nyumbani kwani hana cha kuonyesha zaidi ya pambio na ahadi hewa wale waliomchagua.
Naomba nieleweke Hii ni kwa maslahi ya Wanangara wote na kwa vizazi vyote pasipo kujali misimamo yao kisiasa zaidi ya uwezo wao kiuongozi, bila sisi wenyewe kuiongelea Ngara yetu na wananchi wake, hakuna mwingine wa kuongea na kusikika!
Naomba tu kutahadhalisha Ndugu zangu wa Ngara kuepuka haka kaugonjwa ka uchawa maana naona kameanza kuingia Ngara, sio asili yetu huo, tutawatenga Machawa wote ili mpone kwanza na muelewe uchawa ni udhalilishaji wako binafsi na ndio maana mnasababishana hata teuzi ziwapite wengine!!
Tanzania ni yetu SOTE ikiwamo NGARA! 🤝🇹🇿
*@samruhuza*l
One thought on “Ngara: CCM Tubadili Njia Ndio Tuthaminike?”
  1. Asante kwa uchambuzi mzuri. Mimi Sina megi ila nawapa msemo fikirishi wananchi wa Ngara na kagera kwa ujumla. Wendawazimu ni Kufanya kitu kile kile kwa kurudia rudia, huku ukitegemea matokeo tafauti. Ngara imekuwa chini ya ccm tangu tupate uhuru lakini wananchi wamezidi kuwa masikini mwaka hadi mwaka. Sasa ni mda wa kubadilisha Yale ambayo tumekuwa tu kifanya kwa miaka 60 tangu tupate uhuru. Moja wapo ni ni kudai katiba mpya. Pili ni kubadilisha Chama kilicho utawala kwa miaka yote.

Comments are closed.