Recent Comments

Ngara – Kah, Dharau Zimetosha!

By Baraka Bitariho Sep 5, 2023
Watoto Wengi hawajui kesho yao kama na viongozi wamo kwenye kuzalisha na kukana hivi viumbe ambavyo havina kosa mbele za Mungu. Wanawake tukimkimbilie nani kama hata tuliedhani angetuongoza ana zalisha na kukimbia? Ndio uongozi tulioutegemea kutoka kwa vijana wetu ambao leo wanaondoka na style maluufu kama Mario? Kwa kweli Ngara tunachangamoto nyingi ila sikujua uongozi ilikua nayo ni changamoto moja wapo.
Mwaka 2020 kwenye Uchaguzi mkuu tulimchagua Kijana mmoja ambaye kipindi kile alikuwa hata hajulikani kwa Wananchi.
Tulishawishika kumchagua kutokana na maneno mazuri, ushawishi wa watu waliomtangulia na kutufikia kumtabulisha tukiamini kwamba kwa ushawishi ule tumepata mbunge na kiongozi safi.
Hatukujua kwamba tunaingizwa mkenge masikini!
Baada ya kumjaza kura akashinda, dharau zikaanza.  Ama kweli waswahili walisema JASIRI HAACHI ASILI! Uchaguzi wa 2020 umetutia aibu.
Ni kupitia Uchaguzi huo tulipompata Mbunge kijana mhuni anayetumia Pesa kuwaaminisha Wananchi kwamba yeye ni bora kuliko watangulizi wake, anayetumia nafasi yake kutongoza na kujipatia mademu mpaka wake za watu! Ni mhuni tu
Dharau zake zilivuka mikapa akaanza kuwatimua maswahiba wake waliomsaidia kuingia maarakani, waliomtafutia kura na hata kuchukiwa na jamii kwa namna walivyompambania.
Alitimua madereva watatu, dereva mwingine alifariki. Akatimua baadhi ya waratibu wa kazi zake kuanzia kwenye miradi waliyokuwa wakiisimamia hadi Ofisi ya Mbunge.
Kutokana na hulka yake, aliingilia hata majukumu ya Viongozi wa Wilaya. Akachonganisha na kusambaza umbea juu ya viongozi wakatimukiwa kazi na wengine kuhamishwa vituo.
Kama King Mswatt vile! Akajikusanyia na kuongeza idadi ya Mademu, wengine akanunukiwa magari, kukodishiwa nyumba na kuanzishiwa miradi huku wengine wakiishia kutelekezwa na Mimba na Watoto Wachanga!.
Watoto Wengi hawajui kesho yao kama na viongozi wamo kwenye kuzalisha na kukana hivi viumbe ambavyo havina kosa mbele za Mungu. Wanawake tukimkimbilie nani kama hata tuliedhani angetuongoza ana zalisha na kukimbia? Ndio uongozi tulioutegemea kutoka kwa vijana wetu ambao leo wanaondoka na style maluufu kama Mario? Kwa kweli Ngara tunachangamoto nyingi ila sikujua uongozi ilikua nayo ni changamoto moja wapo.
Ila, nzi hufia kwenye kidonda! Alipotua kwenye Penzi la Mrimbwende wa Kinyarwanda akazama jumla. Alihakikisha familia yao inaongeza idadi ya ng’ombe zizini na hata kufikia kuvunja sheria za Nchi kupeleka mifugo kwenye hifadhi huku akiwa kichocheo cha migogoro ya Ardhi ya Wananchi na Jeshi la Magereza.
Bila aibu na mbele ya Time Kamera Nene, amejigamba sana tuu eti anatembelea Gari la Milioni 700, anajenga nyumba ya Biliobi 1 na Milioni 700 vitu ambavyo sisi hatukumtuma wala hatuvitaki. Kama anavyo ni vyake na havina faida kwa muuza ndizi mbivu pale sokoni wala yule mtoto anayetumia masaa kadhaa kufata maji mtoni.
Sasa, tunakwenda kwenye Uchaguzi. Hatumtaki tena  tunataka Mbunge mwenye uwezo wa kutuunganisha na sio huyu anayejiita MUbunge anayeishi siku nyingi ndani ya mwaka nje ya Wilaya ya Ngara. Mubunge anayedhani ni sifa kukimbia na kuishi mbali na wale waliomchagua; anayedharau maisha ya wana Ngara kana kwamba tunaongozwa kama TV ya Rimoti huku hata nzi hawezi kukimbia akipulizwa mezani kwa upepo na vitisho. Mubunge anatuumiza na taa za ving’ora na kuweka ulinzi kama kwamba kusogelea aliowatongoza na ahadi hewa ni kusogelea ukoma unaoishi kijijini. Analipwa hela zetu zinazokusanywa kama ushuru ila sasa anajenga ukuta mrefu sana kwenye hilo hekaru lake la Bilion 1 ili ajifiche kwa wale anaojidanganya anawaongoza…. ila anaowaongoza ni wale anaoishi nao wakimlia pesa kule mumahanga; pesa ambayo ni jasho la wana Ngara.
Ngara iwe kitovu cha Uchumi wa Afrika Mashariki. Nchi jirani za Rwanda, Burundi, DR Congo, na hata Uganda wachukue bidhaa kutoka kwetu.
Ngoma ya watoto haikeshi. Mbunge wetu hawezi. Anachokijua ni kupiga kelele, kutudanganya kwamba miradi ametekeleza yeye kana kwamba hatuna Serikali??? Dharau.
Dharau, fitina, uchonganishi ni sifa zake. Tumpumzishe huyu Mubunge ili aendeleze anavyopenda maana Wilaya ya Ngara si moja ya kitu anachopenda maana hata hayo mamilioni anayolipwa yanaishia huko anapoishi na anapotesa kwa starehe za ujanani.
Kwa kweli huyu MUbunge anavituko na tungoje tujipatie Mbunge atakayeishi nasi, atuongoze akiwa kwenye jamii yetu.
Wakati tunamchagua alitudanganya kwamba ni agizo kutoka juu, tukaamini kwamba tunakwenda kupata muwakilishi walau Uteuzi utamhusu awe hata Naibu Waziri au Waziri, kumbe ni muongo!.
Eti ni agizo kutoka juu!!! Juu ya vifua vya mabinti na wake za watu ama ni agizo nyuma ya kuta ndefu zinazoficha madhara ya ahadi hewa na uso wa kiongozi aliyeongeza idada ya watoto waliotelekezwa kwenye jamii? Basi tuendelee kushuhudia majigambo na dharau tulizojiletea kwa kuchagua tuliedhani angekua kimbilio la jamii akaishia kuikimbia Ngara. Aendelee kuja na kushitua shitua jimboni na kuogopa eti waliomchagua kwa moyo mmoja ni wajihami na watu waliomchagua.
Hizi “ndizo dharau ambazo zimewachosha wana Ngara,” wanawake wawili waliokutwa waikisubiria usafiri sokoni walivyomwambia Kamera Nene na Timu Yake.