Recent Comments

Ngara ya Vurugwa, Kisa Madaraka

By Baraka Bitariho Jan 27, 2024
Rulenge, Kagera - wafanyabiashara wakiwa sokoni

NDAISABA UNAIVUTUGA NGARA HATA KAMA NI UCHU WA MADARAKA HAPANA!

 

Rulenge, Kagera – wafanyabiashara wakiwa sokoni
  • Serikali ya Tanzania chini ya Amiri jeshi Mkuu Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza Miradi ya maendeleo kama ilivyo kwenye majimbo mengine.

Huko Wilayani Ngara Kuna Mbunge kazi yake ni kudangaya Umma kwaajili ya kutafuta huruma ya Wananchi kuwa kila kinachofanyika ni yeye anafanya, aibu.

Tangu zoezi la ufungaji wa taa linakaribia kuanza Mbunge na wapambe wake waliowekwa kila kona ya Ngara walikuwa wakijadili namna yakutumia fursa hiyo Kisiasa.

Badala ya kusema mazuri ya Serikali na Chama chenye Ilani yeye anawaingiza Chawa kwenye mkenge wa ndiyo Bwana

Hivi ni lini Ngara itakuwa kama wengine wanaojua kuwa Mbunge Hana uwezo wa kufunga taa,kujenga lami,kuanzisha viwanda,kuweka maji na Umeme labda tu kujenga Ushawishi kwa Serikali?

Wananchi msipogutuka na kupinga ipo siku atawadanganya na Upepo mnaovuta anawapa yeye, au Maporomoko ya Rumumo na Madini ya Nickel alileta yeye

Yeye ana uwezo gani kuliko wengine Mbona majimbo mengine hatujawahi kusoma wala kusikia upuuzi wa majigambo?

Na vipi waliokuwa Wabunge wa Ngara wamelala ? Au wao waliemda kulala!

Kamera Nene imechelewesha picha za Rulenge, turazipata tu.