Moja ya mafanikio ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ni kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar na kuzika chuki za kisiasa. Shein ambaye ameingia madarakani mwaka 2010 zamefanikiwa kurudisha hali ya amani na utulivu katika visiwa vya Zanzibar. Mafanikio hayo yamekuja baada ya Shein kutekeleza matakwa ya kikatiba ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Cilil Union Front (CUF) vyeye uwakilishi katika Baraza la kutunga sheria.
Ni ukweli usiopingika kwamba mara baada ya Zanzibar kufanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi katika mwaka 1995 ufa mkubwa ulijitokeza ambapo chuki za kisiasa ziliibuka na wananchi kugawanyika. Machaguko ya kisiasa yalisababisha ndugu wa damu kushindwa kuzikana pamoja na kutembelea huku waumini wa dini ya Kiislamu walio wengi Zanzibar wakigomea hata kufanya ibada katika misikiti kwa sababu tu kwamba huu unatumiwa na wafuasi wengi wa chama fulani.
Juhudi mbalimbali zilichukuliwa na jumuiya za kimataifa ikiwemo Jumuiya ya Madola kwa lengo la kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar na kuacha siasa za uhasama. Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Kikwete mara kadhaa alisikika akisema anasononeshwa na mpasuko wa kisiasa Zanzibar na kusemaSerikali ya Umoja wa Kitaifa ndiyo pekee itakayowaunganisha wananchi wa Zanzibar na kuishi kama zamani.
Hali hiyo ilisababisha wananchi wa Zanzibar kupiga kura ya maoni Mwaka 2010 na kuamua hatma ya kisiasa kuhusu kuwepo kwa Serikali ya umoja wa kitaifa ambayo ilionekana kama ndiyo muarobaini wa matatizo ya kisiasa kwa mujibu wa utafiti wa makundi mbali mbali na wanasiasa na jumuiya za kimataifa. Matokeo ya kura ya maoni yalionesha kuwa asilimia 66. ya Wazanzibar walitaka kuwepo kwa muundo wa Serikali ya Umoja wa kitaifa huku asilimia 33% wakipinga mfumo huo.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Shein iliridhia kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa kuzingatia demokrasia maamuzi yanayofanywa na wengi. Rais Dk. Ali Mohamed Shein ameingia katika kumbukumbu ya kuwa rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibzar kutumia mfumo wa muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuunda Serikali inayowashirikisha wapinzani.
Akizungumza katika mikutano wa kampeni za kisiasa katika visiwa vya Unguja na Pemba, Shein, anasema akifanikiwa kuingia madarakani tena kwa awamu ya pili atahakikisha anatimiza matakwa ya kikatiba kwa kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa. Shein anasema Serikali ya umoja wa kitaifa ni matokeo ya uamuzi wa wananchi wa Zanzibar ambao walipiga kura na kutaka kuwepo kwa ajili ya kumaliza chuki za kisiasa.
Alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa anayoiongoza yeye kwa kiasi kikubwa imeondoa siasa za chuki na uhasama na kuwaunganisha wananchi wa Unguja na Pemba na kuwa kitu kimoja. âMoja ya mafanikio makubwa ya Serikali yangu ninayoiongoza ikiwa na muundo wa Serikali ya umoja wa kitaifa ni kuzika chuki za kisiasa kwa kuwaunganisha wananchi wote wa Unguja na Pemba na kuwa kitu kimoja,â anasema Shein.
Anasema akifanikiwa kupata ridhaa ya wananchi wa Zanzibar ya kuwa Rais kwa awamu ya pili atahakikisha anaunda Serikali itakayojumuisha vyama vya siasa vilivyomo katika Baraza la Wawakilishi. Shein amewakumbusha wananchi na viongozi wa vyama vya siasa kulinda na kudumisha amani na utulivu kwa nguvu zote kwa ajili ya faida ya wananchi wa Zanzibar.
Anasema athari za vurugu za kisiasa na chuki zilizokuwepo awali wananchi ni mashahidi wameziona wenyewe kwa hivyo wakatae aina yeyote ya ushawishi unaoweza kusababisha uvunjaji wa amani. âWananchi msikubali kushawishiwa kuingia katika vurugu za kisiasa ambazo madhara yake ni makubwa huku viongozi na nyinyi mnalazimika kulinda ndimi zenu katika matamshi mnayoyatowakatika majukwaa ya kisiasa,âShein anasisitiza.
Kisiwa cha Pemba ambacho kiliathirika na siasa za chuki sasa kimebadilika kabisa ambapo wafuasi wa vyama viwili vya siasa vyenye upinzania CCM na CUF wakionekana kufanya siasa katika njia za kiungwana kabisa bila ya kupingana. Rais mstafu wa Zanzibar wa awamu ya nne Abeid Amani Karume akizungumza katika mkutano wa hadhara hapo katika uwanja wa demokrasia, anasema amani na utulivu uliopo sasa ulichukuwa muda mrefu hadi kuimarika na wananchi kufaidi matunda.
Karume anasema viongozi wakuu wakiwemo rais Jakaya Kikwete walishiriki katika kufanya mazungumzo ya kuleta amani hiyo kwa kufunga safari kuzunguka dunia nzima na kuahidi kwamba wananchi sasa wapo wamoja. âWananchi amani iliopo sasa ilichukuwa muda mrefu kuja kwa kuwaunganisha wananchi na kuwa kitu kimoja…..msikubali kuichezea kwa kupokea vishawishi vya aina mbali mbali vitakavyovunja umoja huo,âanasema Karume.
Makamo wa kwanza wa rais anayeunda Serikali ya umoja wa kitaifa maalim Seif Sharif Hamad pia anasema akichaguliwa kuwa rais wa Zanzibar ataunda Serikali ya umoja wa kitaifa. Akizungumza katika mkutano wa hadhara, katika uwanja wa urafiki mjini hapa, Hamadi anasema Serikali ya Umoja wa Kitaifa ina faida kubwa kwa kuwa inaunganisha wananchi na kuifanya nchi iwe na hali ya utulivu, amani na mshikamano.
âNikichaguliwa kuwa rais wa Zanzibar nitahakikisha kwamba naunda Serikali ya umoja wa kitaifa kwa ajili ya wananchi wote kwani faida zake ni kubwa tumefaidika nazo sote, anasema Hamad. Muundo wa Serikali ya umoja wa kitaifa uliopo Zanzibar umepata mafanikio makubwa huku washiriki wa maendeleo pamoja na jumuiya ya Ulaya wakisisitiza kwamba ndiyo njia pekee ya kumaliza siasa za chuki Zanzibar.
Balozi wa jumuiya ya Ulaya nchini Filiberto Ceriani Sebregondi anasema amani na utulivu uliopo Zanzibar chini ya Serikali yaUmoja wa kitaifa ni mafanikio makubwa ambayo baadhi ya nchi zenye migogoro zinatakiwa kuiga .
âJumuiya ya Ulaya na nchi marafiki zimefurahishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa chini ya mfumo wa umoja wa kitaifa kwamba imepata mafanikio makubwa kwa kuondowa siasa za chuki na uhasama huku nchi nyengine zenye migogoro zinatakiwa kuiga mfano wa Zanzibar,â anasema Sebregondi.
Jumuiya ya Ulaya ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa mstari wa mbele kufuatilia hali ya kisiasa Zanzibar pamoja na kutoa misaada mingi katika sekta mbali mbali ikiwemo miundo mbinu ya bandari na barabara.
OP Habari Leo
Recent Comments