Kijana ni nguvu kubwa ya siyo baadae na hata sasa, hii ndiyo sababu inayofanya niongee na kijana kila siku yani jana kijana leo kijana na hata kesho nikiwa hai ntaongea sana na kijana sijajua tafsiri nzuri ya kijana ni nani hasa katika umri ila kwangu ujana ni umri wa miaka 15 hiviii mpaka 40 hapa mtu anastaili kuitwa kijana sasa leo nitakupa vitu vinavyomkwamisha kijana asipate mafanikio.
1: Matumizi mabovu ya muda, vijana wengi wamekuwa wakitumia muda hovyo na kushindwa kutimiza mambo katika maisha yao, vijana wengi hawajui muda sahihii wa kula bata,muda wa kazi hali inayokwamisha maendeleo yao kiujumla.
2: Nidhamu, Vijana wengiwamekuwa na nidhamu ndogo sana hasa katika utafutaji na matumizi ya pesa mtu anatumia pakubwa kuliko pato lake hili ni tatizo kwa vijana wengi huwa wanafanya biashara nakutafuta pesa kwa nguvu lakini mwishowe kuishia kutumia kwa anasa kunywea pombepia kuhongea wanawake na mengine mengi na kufanya kukwama kwakuwa hawakuzi uwekezaji pia akiba ni ndogo mno au hakuna kabisa.
3: Haraka ya Mafanikio, vijana wengi wanakosa uvumilivu wanatamani kufanikiwa haraka bila changamoto wala kujipa muda hali inayopelekea kuishia pabaya kwenye ushirikina pia shughuli haramu ambazo huwacost na kufanya ndoto za kufanikiwa kufa kabisa.
4: Papara, pia vijana huwa hawatulii na kujipa muda kufanya mambo hali inayopelekea kushika mara kile mara muuza mitumba mara kitimoto, mara mgahawa yaani huku kule hali inayopelekea kuharibu mtaji na kufeli kuendelea.
5: Kutokukubali maisha yao, vijana wengi hufeki maisha na hata kuiga maisha ya wengine ili tu waonekane wana uwezo ambapo hii huwaathiri vijana wengi na kupelekea matumizi makubwa bila kipato na kusababisha madeni,kuharibu biashara na kupelekea kufeli kinaendeleo.
Nikukumbushe tu kiuhalisia maisha yana kanuni moja hakuna nyingine ni kuwana na bidii ufanikiwe mafanikio hayatoki mbinguni unayatengeneza mwenyewe.
Recent Comments