SI vitisho na matusi, wala madai ya kuwa yeye Frederick Sumaye alihama CCM na kuhamia UKAWA kwa kutafuta cheo, vitakavyomtoa nje ya mstari wa kumuunga mkono Edward Lowassa kuleta mabadiliko nchini. Anaandika Jabir Idrissa ⦠(endelea).
â
Sumaye ambaye ni waziri mkuu mstaafu aliyetumika wakati wa serikali ya awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa, amesema hayo akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya ubunge jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Sumaye, mwanasiasa gwiji aliyekuwa waziri mkuu vipindi viwili mfululizo âNovemba 1995-2005, alishiriki uzinduzi wa kampeni akimnadi mgombea anayewakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Saed Kubenea.
Sumaye na Kubenea wamekuwa marafiki kiasi cha Kubenea kuongoza mkutano wa waandishi wa habari hotelini Hyatt Kilimanjaro, Dar es Salaam, ambao Sumaye aliutumia kutangaza nia ya kuwania uteuzi wa kugombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Baada ya kukatwa jina lake, kama alivyotendwa Lowassa, Sumaye hatimaye alihama CCM na kujiunga na UKAWA kwa lengo la kuharakisha mabadiliko ya kuiondoa CCM madarakani.
Akihutubia mkutano uliofanyika viwanja vya Faru vilivyoko njiapanda ya Mabibo, Sumaye amesema hatafuti cheo kama CCM wanavyomtuhumu, kwa kuwa alikuwa waziri mkuu, wadhifa atakaoupata tu aliyechaguliwa mbunge jimboni wakati yeye hagombei ubunge.
Kadhalika amesema hawezi kuwa rais kwa sababu Lowassa ndiye mgombea urais kupitia Chadema anayewakilisha UKAWA.
âSitafuti cheo kwa sababu kuna cheo gani tena mimi zaidi ya urais ambao tayari tunaye mgombea Lowassa. Waziri mkuu siwezi kuwa kwa sababu sikugombea ubunge. Nimejiunga na UKAWA kuleta mabadiliko kwa kuiondoa CCM madarakani,â amesema.
Sumaye pia aligusia mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi jijini Dar es Salaam, akisema amradi huo ni wa kifisadi ambao hautapunguza msongamano kwa kuwa barabara hazitoshi.
Amempamba Kubenea akisema ni kijana mpenda haki aliyejitolea maisha yake kupigania haki za Watanzania, hata kufikia kufungiwa gazeti lake na serikali ya CCM kwa sababu wakiandika ukweli wa maovu ndani ya serikali.
Kubenea amesema akiingia bungeni atapigania kurudisha kwa wananchi Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambalo limeuzwa kifisadi chini ya usimamizi wa mgombea mshindani wake Ubungo, Didas Masaburi wa CCM.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alihudhuria kwa muda mfupi mkutano huo na kusema wananchi wa Ubungo wamepata mbunge mwingine mahiri atakayewawakilisha vizuri bungeni.
Recent Comments