Kampuni za Apple na Google Marekani zinapanga kuleta software ya simu za mkononi ambayo inaweza kumpa taarifa Mtu yeyote anapomkaribia Mtu mwenye virusi vya corona, mwezi May walitoa software ya namna hiyo kwa ajili ya kutumika kwenye Nchi 22 lakini hii ya sasa imeboreshwa na ni rahisi zaidi.
Itavyofanya kazi, kwanza Mtumiaji lazima airuhusu kufanya kazi kwenye simu yake ambapo Wagonjwa wa corona watakua wanaongozwa kujisajili kwenye simu zao na Mamlaka za Afya hivyo simu zao zinapomkaribia Mtu mwingine yeyote mwenye hiyo software atapata taarifa.
Mamlaka za Afya zitatakiwa kutoa ruhusa ya kutumika kwa software hii kabla ya kuwafikia Watumiaji mtaani ambapo hadi sasa sehemu kama Virginia, Washington DC, Nevada na Maryland zote za Marekani zitakua za kwanza kupata update za hiyo software.
Mpaka sasa Marekani ndio Nchi inayoongoza kwa vifo vingi vya Watu vilivyotokana na virusi vya corona ambapo waliofariki Marekani pekee ni zaidi ya laki moja na elfu themanini na nane Wagonjwa zaidi ya milioni 6 huku Nchi ya pili kwa vifo ikiwa ni Brazil yenye vifo laki moja na elfu ishirini na mbili na Wagonjwa ni zaidi ya milioni tatu laki tisa, India ikiwa ya tatu kwa vifo zaidi ya elfu sitini na sita na Wagonjwa zaidi ya milioni tatu laki 7.
Recent Comments