Recent Comments

Tulipotoka, Tulipo, na Tuendapo Twakufahamu?

By Baraka Bitariho Dec 25, 2023
Mwanafunzi, kijana maridadi akiwa na heshima zake kwenye jamii, wazazi, na akiwa anajitafuta. Leo hii ni mtafuta maadui na kuwa k Mkasi wa kuchana chana jamii baadala ya kuunganisha jamii na kukumbatia udongo uliomtunza na kumkumbatia kipindi anajitafuta. Hata makazi alishahamisha kwa kuogopa hali ilivyokua Jana. Pengine mikakati ya maisha ya kesho ameshaiweka vizuri kwani leo hata kuhudhuria mikutano yake unapatia 40-40 ili usimamishe njaa ya leo badala ya kuunda mikakati itakayokuwezesha kuoiga mbizi katika dimbwi utakalokutana nalo kwenye maisha ya kesho.

Katika pita pita zangu nikakutana na huu ujumbe, pengine unanihudu mimi, wewe msomaji, ama mlengwa yeyote aliyeshau kuwa Leo ni Tamu kuliko Jana ila Hana uhaka na kesho yake. Usomapo hii makala, chukua muda, tafakali na jiulize kuwa anayeongelewa sio mimi ama sijafanya maamuzi kama haya na kwa kuwa hamna kati yetu mwenye uhakika na kesho, basi tujitathimini kama tuyafanyayo yanatubeba leo na kesho ili kesho yetu itupokee vizuri.

 

Makala ilianza kama ifatavyo…

 

*RUHORO UMESAHAU ULIKOTOKA, HAUJUI UNAPOKWENDA. PICHA HII NA UJUMBE HUU VIKUSAIDIE KUPUNGUZA KIBURI.*

Kwa kuzingatia Ibara ya 12(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikisomwa sambamba na imani nambari 2 katika mtiririko wa imani 3 za Chama cha Mapinduzi inayotamka bayana kwamba *”Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake”*

Ninapenda kutoa maoni yangu kuhusu kauli yako uliyoitoa hivi karibuni katika group la Jimbo inayokebehi na kudharau Wajasiliamali na Wafanyabiashara kwamba hawawezi chochote zaidi ya kuuza dompo na bisukuti, dhihaka hiyo akiitoa kwa kiburi cha utajiri wako. Wafuasi wako wanaendelea kuitumia kauli hiyo kama dhihaka na tusi kwa kuwasakama Wajasiriamali kwa kuwa umewaaminisha kwamba wauza dompo na bisukuti ni watu duni wasiostahili heshima katika jamii.

Kauli kama hizi kutolewa na Kiongozi uliyeaminiwa na Chama cha Mapinduzi na kupewa dhamana kubwa ya kuwa mwakilishi wa Wananchi, zinawaudhi wengi katika jamii kwa kuwa Wananchi walio wengi wanajitahidi kufanya bidii katika kujikwamua kiuchumi ikiwemo kufanya biashara ndogondogo, za kati na kubwa ili kuhudumia familia zao na kushiriki katika ujenzi wa Taifa kwa njia ya kulipa kodi. Ni vyema kukumbuka kuwa utajiri wako haupaswi kuwa sababu ya kutoonesha heshima na kutokuthamini utu na ubinadamu wa watu wengine katika jamii. Wauza dompo na bisukuti, kama walivyo wajasiriamali wadogo na Wafanyabiashara wengine wanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua uchumi wa Taifa letu kwa hiyo hawapaswi kupuuzwa au kudharauliwa.

Labda unaweza kuwa umesahau kutokana na madaraka yaliyokulevya, kiburi cha uzima na utajiri ulio nao kwa sasa. Lakini ikiwa utakumbuka vizuri wakati unafanya kazi Upendo lodge Rulenge hakuna aliyewahi kukudharau, kukudhihaki na kukukejeli kutokana na kazi yako. Hakuna aliyewahi kukudharau na kukukejeli kwamba jina Ndaisaba George sio la kwako bali ulilipata kwa kusaidiwa na Mwalimu Kazi Rusabi ulipoenda kurudia Shule ya msingi huko Mabawe. Hakuna aliyekudharau kwa kwenda kurudia Shule na kununua jina wala kwa kazi ya kutandika vitanda na kuuza vinywaji kwa Wateja Upendo Lodge kwa kuwa watu walithamini na kutambua juhudi zako za kujikwamua kijamii na kiuchumi. Iweje leo uwadharau watu na uwalipe vijana wawakejeli mitandaoni kwa kazi zao zinazowapatia mapato halali?

Ni muhimu kutoa kauli zenye heshima kwa kila mwananchi bila kujali hali yake. Kauli zenye dhihaka zinaweza kuleta mgawanyiko na kuvuruga amani ya kijamii. Nashauri utumie nafasi yako ya Ubunge kama kiongozi wa Wananchi kujenga daraja la maelewano katika jamii bila kujali wale walio na mafanikio na wale wanaojitahidi kujikwamua kiuchumi. Kwa kufanya hivyo, utaonesha uongozi wa kiungwana na kuleta mabadiliko chanya katika mtazamo wa jamii kwa wajasiriamali wadogo.

 

 

Mwanafunzi, kijana maridadi akiwa na heshima zake kwenye jamii, wazazi, na akiwa anajitafuta. Leo hii ni mtafuta maadui na kuwa k
Mkasi wa kuchana chana jamii baadala ya kuunganisha jamii na kukumbatia udongo uliomtunza na kumkumbatia kipindi anajitafuta. Hata makazi alishahamisha kwa kuogopa hali ilivyokua Jana. Pengine mikakati ya maisha ya kesho ameshaiweka vizuri kwani leo hata kuhudhuria mikutano yake unapatia 40-40 ili usimamishe njaa ya leo badala ya kuunda mikakati itakayokuwezesha kuoiga mbizi katika dimbwi utakalokutana nalo kwenye maisha ya kesho. Je kama Jana ilikua chungu kuliko leo yako, hizi poza njaa, 40-40 zitaichongaje kesho yako? Fikiria na tafakali ukiwa unapokea hizi punguza njaa unapohudhulia mikutano yake na kingine kweli ni lazima ulipwe ndio utukuze na kupiga vigere gere ama ndio njia ya kuuza kesho yako kww huyu aliyesau Jana yake kama picha inavyoosha hapo juu?

Chama kilichokupa udhamini kinasisitiza misingi ya haki, usawa, udugu na heshima kwa kila raia. Kukashifu wajasiriamali ni udhaifu wa kiuongozi na ni kinyume kabisa cha misingi ya CCM. Uongozi wako unatakiwa kulenga maendeleo na ustawi wa jamii na unapaswa kuwa mfano bora wa kuigwa, ukitetea usawa na kuthamini mchango wa kila mwananchi. Ninakusihi utumie mamlaka yako kukuza misingi ya uongozi bora, kuheshimu watu wote, na kufanya kazi kwa bidii kuleta umoja na maendeleo kwa nchi yetu.

Ninatumaini utazingatia maoni haya na kuyapa uzito unaostahili, akhsante!

 

Jumbe iliyoazimwa iliishia hapo. Tafari na fikilia, je huu ujumbe unakugusaje kwenye maisha yako, maisha ya qanao, na wajuu zako? Na wewe umejisahau ama?