Recent Comments

TUMIENI VYOO ACHENI KUJISAIDIA VICHAKANI.

By Mwafrika Jan 9, 2024

NA,ANKO G

Wakati serikali ikihamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo safi na salama, bado kuna baadhi ya wananchi wilayani Ngara mkoani kagera wanakaidi na kuendelea kuchafua mazingira kwa kujisaidia vichakani (Haja kubwa na ndogo) jambo ambalo ni hatari kwa afya ya binadamu.

Kwa jiografia ya eneo la Ngara eneo kubwa linachukuliwa na misitu/mashamba kiasi kwamba siyo rahisi kukuta aridhi ambayo ni tupu.

Katika maeneo ambayo mazao ya vyakula hayasitawi vizuri hupanda miti huku katika maeneo yanayo stawisha vyakula yakilimwa mazao ya vyakula.

Vilevile Ngara inaundwa na milima na mabonde ambapo baadhi ya mabonde huzalisha maji ambayo pia hutumika kwaajili ya matumizi ya majumbani kwani maeneo mengi bado hayajafikiwa na miradi ya maji.

Aidha kumekua na tabia inayo endelea mpaka sasa ambapo baadhi ya watu ambao hujisaidia vichakani ambapo ukipita katika maeneo mengi yenye misitu ya vinyesi vinaonekana kutapakaa hali ambayo ni hatari kwa afya za watu.

Ikumbukwe kuwa kinyesi kuzalisha magonjwa mbalimbali na hata mvua inapo nyesha basi mvua huhamisha kinyesi kilipo na kuelekea mabondeni ambapo kuna mito ambayo wanachi huchota maji na kutumia majumbani hali hiyo inaweza kusababisha magonjwa mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa kinyesi kinaweza kusababisha magonjwa kama vile; Kipindupindu,Ugonjwa wa kuhara,Minyoo ya safura, Homa ya matumbo(Taifod), Amiba na magonjwa yanayo fanana na hayo.

Hali hii inaweza chukuliwa kama hali ya kawaida lakini kunisaidia vichakani kunahatarisha maisha ya watu wengi licha ya watu kuchukuliwa kama suala la kawaida.

Imekua kama utamaduni wa muda mrefu ambapo imekua kama ugonjwa wa kirithi kwani siyo watoto tu wanao jisadia maporini bali kuna watu wazima hufanya hivyo.

Kama ambavyo maneo mengine wamefanikiwa kukomesha tabia hizo kuna haja ya kukomesha tabia hiyo kwa kuweka sheria kali na faini kwa anae bainika kufanya hivyo hii iwe kwa serikali na hata wamiliki wa maeneo/mashamba na misitu.

Jamii iliyo bora ni jamii yenyewe afya jukumu la usafi wa mazingira linamhusu kila mtu.