Na,Mwandishi wetu-Bukoba – Mkoa ambapo moja ya rishe bora ni senene na kumbi kumbi
Ilikuwa miaka,miezi, majuma, siku na sasa yanahesabika msasaa kadhaa kabla ya Wanachama wa CCM mkoani hapa kuamua kusuka au kunyoa.
Ikiwa ni msiba hapa ndipo busara na maamuzi ya kiutu uzima yanapotakiwa kufanyika na ndipo utasikia maamuzi ya kuzika au kusafirisha.
Siku chache zilizopita niliandika kuhusu Uchaguzi huu unaokwenda kufanyika na nikauliza Kama wana CCM KAGERA WANATAKA KUMKABIDHI CHAMA MTUHUMIWA WA UFISADI.
Japo niliyemzungumzia kutokana na vyanzo vingi vya habari hakusema chochote nilishambuliwa sana kwa maneno na wafuasi wake. Kweli nawashukuru ila yote yanaonyesha ni namna gani matumbo yana njaa.mliojipa nafasi za usemaji aka wapuriza zumari mliropoka mengi acha kabisa
Sasa tunahesabu masaa. Kulia na kucheka zote ni kelele. Acha niwaletee wasifu wa Karamagi leo. Nikipata nafasi kesho nitamzungumzia Mgombea mwingine wa nafasi ya Mwenyekiti Bi. C. Buhiye ambaye wapambe wa Kigogo Karamagi mnajaribu kumpaka matope mkidhani hana nguvu. Eleweni uongozi wa kuchaguliwa ni mchezo wa kubadilishana.
NAZIRI MUSTAFA KARAMAGIÂ alizaliwa tarehe 13.12.1953Â Kijiji cha Nyakabanga,Kata ya Butelankuzi Wilaya ya Bukoba Vijijini; Mkoani Kagera.
Mzee karamagi ni miongoni mwa wasomi wazuri wa taifa hili kwani alipata Elimu ya Msingi kwenye Shule ya Rubale, Elimu ya Sekondari alisoma Shule ya Nyakato maarufu kama Kagara kuanzia kidato cha 1 mpaka cha 4 na kidato cha 5 mpaka cha 6 Shuke ya Sekondari Kibaha.
Alifanikiwa kupata Elimu ya juu katika vyuo mbalimbali Duniani kikiwemo Chuo Kikuu cha Madini cha St Petersburgh huko Urusi, Edimburgh (Uingereza) na Strathclyde (Uingereza). Huyu Bwana ni Msomi haswa. Bingwa katika masuala ya madini,Uhandisi Mitambo na Uchumi na Fedha.
Wakati Karamagi akichuana na wenzake kugombea Uongozi kwenye Chama tawala, Wananchi wanatakiwa kujiuliza maswali mengi alisahau nini wakati akiwa mtumishi?
Ikiwa kweli alikuwa na nia ya kuiendeleza Kagera kwanini hakufanya hivyo walau akiwa Mbunge wa Bukoba kipindi kile Chama kilimpomteua kupeperusha bendera ambapo aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko na baadaye kuhamishwa wizara na kuwa Waziri wa Nishati na Madini?
Ni huyo huyo Nazir Karamagi ambaye wapuriza Zumari wanaimba sifa kedekede kwamba ni mjasiliamali na mwekezaji aliye bobea! Kama aliwahi kuwa Mkurugenzi katika Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), na mpaka sasa ni mjumbe wa Bodi mbali mbali za kitaifa na kimataifa amesaidia vipi kuwakwamua wananchi ambao Umasikini unawapeleka puta?.
Nilipoandika kuhusu zile tuhuma,nikashambuliwa kwa maneno na kejeli za wapambe kunammoja wao alimnadi Nazir Karamagi kwamba amewekeza katika miradi mbali mbali ikiwemo makampuni yaliyomo katika Soko la Mitaji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Stock Exchange), katika kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services Ltd (TICTS) kampuni inayoendesha kitengo cha makontena katika Bandari Kuu ya Dar es Salaam, kampuni ya Tanzania Microfinance inayo shughulika na kutoa mikopo kwa wafanyakazi na wajasiliamali wadogo wadogo. Sasa mimi nawewe tushirikiane kama kweli anakopesha ameshindwa kuwakopesha wananchi wa kule Bukoba Vijijini?
Ameshindwa kuwakopesha wananchi wa kule Kyerwa,Karagwe,Ngara, Biharamulo na Muleba?
Kipindi Fulani katika Kampeni cha Uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi Mkoani Kigoma nilimsikia Mhandisi Christopher Chiza akitafsiri neno Injinia. Alisema âAn engineer is a professional who is involved in inventing, designing and maintaining a variety of machines, structures and data systemsâ. Engineers are experts in their fields, creating and innovating constantly.
Kwa lugha rahisi tunaweza kusema Mhandisi ni mtu mwerevu anayeweza kubuni,na kutumia maarifa yake kwaajili ya kutatua au kutafuta suluhu ya changamoto za maisha yake na wanaomzunguka. Siyo sifa za wapambe wachumiatumbo kama tunaowatazama leo.
Binafsi,kwa uhuru wa kikatiba bila kuathiri mawazo ya wajumbe ningependa kuwashauri kukumbuka kuwa Mkoa wa Kagera kwa sasa unakabiliwa na changamoto ya umaskini licha ya uoto wake wa asili kuwa mzuri sana,na mazingira yote kuruhusu uwekezaji wa kila aina. Tatizo bado lipo kwa Viongozi wanaotanguliza masilahi yao mbele.
Siku za nyuma kidogo tu, tumemshusudia Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa Ziarani kwenye mataifa mbalimbali Duniani akifungua milango ya uwekezaji. Mkoa wa Kagera una mikakati gani ya kusafirisha bidaa? Hayo ni mambo ambayo wagombea wetu wanatakiwa kujiuliza.
Nimeanza kwa kusema Wana CCMÂ Kagera kusuka au kunyoa. Kufanya maamuzi sahihi kwaajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo,vinginevyo lawama zitawaandama kwakukubali kuburuzwa
Sisi www.simamia.com na simamia TV tunawatakia Uchaguzi mwema kwaajili ya kuwapata Viongozi wanaokidhi vigezo vyote kwa sifa na uzoefu ili kuleta mabadiliko chanya kiuchumi kwa maendeleo ya Mkoa wetu wa Kagera.
Recent Comments