Recent Comments

UCHOMAJI MISITU UNAGHARIMU MAISHA

By Simamia Ngara Jul 31, 2024
Exif_JPEG_420

NA,ANKO G.

Wilaya ya Ngara na mkoa wa Kagera kwa ujumla ni mkoa ambao wakazi wake wanamwitikio mkubwa wa upandaji miti ambayo inakuza uchumi wa Kagera na kusaidia kudhibiti mabadiliko ya haliyahewa.

Licha ya kuwa na mwamko huo bado kuna baadhi ya watu wasio na nia njema wanao choma misitu hovyo hasa kipindi cha kiangazi.

Aidha simamia.com imefika katika eneo la Kijiji cha Ibuga, kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera na kushuhudia eneo la msitu likiwa limeteketea kwa moto.

Hata hivyo kitendo hiki kianaathiri uchumi wa aliepanda msitu huo kwakua tayari anaingia hasara ya kiuchumi pamoja na kuathiri watu wanao zunguka eneo hilo kutokana na uharibufu wa mazingira na hali ya hewa.

Hivyo basi watu wanatakiwa kuachana na vitendo vya uchomaji misitu hovyo kwasababu vitendo hivyo vinagharimu maisha ya watu kiuchumi na uhai kwasababu binadamu wanategemea hewa safi kutoka kwenye miti na ndiyo maana Dunia nzima ina sera ya kukata mti na kupanda mti.