WAKATI kampeni zikiwa zinaendelea kwa kasi katika jimbo la Dodoma Mjini, lakini kwa vyama vingine havijaanza kampeni hadi sasa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha kwa vyama hivyo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma ⦠(endelea).
Zikiwa zimebaki siku 37 kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu, lakini hadi sasa ni CCM na UKAWA pekee ndiyo wanaofanya kampeni katika jimbo hilo, huku vyama vingine hazijazindua kampeni zake hadi sasa.
Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha UDP wilayani hapa, Azimio Tarota amesema hawajaanza kampeni kwani wanasubiri utayari wa mgombea wao, Catherine Mhando.
Amesema chama chao kinamsubiri mgombea wao akishakuwa tayari kuanza kampeni atawataarifu wanachama wao ili kuanza kumnadi kwa wapiga kura.
Naye, Katibu wa Chama cha UPDP mkoni Dodoma, Mohamed Bakari amesema mgombea wao ubunge, Runna Kaliya anatarajiwa kuanza kampeni wiki ijayo.
âMakao Makuu bado hawajatuletea fedha. Wamesema tutafanya uzinduzi wiki ijayo ambapo mgombea urais atakapokuja mjini hapa ili aweze kutuzindulia pia kampeni zetu za ubunge,âamesema.
Katika hatua nyingine chama cha CHAUMA kinatarajiwa kuanza kampeni zake za ubunge,
Septemba 19 ( Ijumaa wiki hii) katika viwanja vya Majani ya Chai mjini hapa, kumnadi mgombea wake wa ubunge Godfrey Nastory.
âBado hatuajaanza kampeni kwa sababu ratiba zimeingiliana na mambo ya kitaifa,âamesema Katibu wa Chausta mkoani hapa, Alfonce Mayunga.
Alipoulizwa kuhusiana na muda wa kuliobakia kama unatosha kuzunguka kata zote 41, Mayunga amesema Chausta haitegemei ruzuku kuendesha shughuli zake za kisiasa.
Jumla ya vyama saba vimesimamisha wagombea ubunge katika jimbo la Dodoma Mjini, lakini vyama vya CCM na Chadema ndiyo zilizoendelea na kampeni zake.
Recent Comments