Recent Comments

UNESCO: WATOTO MILIONI 258 DUNIANI HAWAKWENDA SHULE MWAKA 2018

By ObyMack David Jun 23, 2020


UNESCO: WATOTO MILIONI 258 DUNIANI HAWAKWENDA SHULE MWAKA 2018

Ripoti mpya ya hali ya elimu duniani ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) imesema watoto milioni 258 hawakwenda shule mwaka 2018, sawa na 17% ya vijana ulimwenguni

Takriban asilimia 90 ya vijana walioathiriwa zaidi ni kutoka nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia. Umasikini umetajwa kuwa ndio haswa unaoathiri fursa za elimu

Ripoti hiyo pia imeeleza kwamba mamilioni ya wavulana na wasichana wanabaguliwa katika mifumo ya elimu kwa sababu ya asili zao au ulemavu walionao

Aidha, ripoti hiyo imebaini kuwa katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati, watoto wenye ulemavu, kwa 19% wapo chini ya kiwango cha kuhudhuria masomo

Imesema makundi yenye matatizo mbalimbali yanawekwa au yanasukumwa nje ya mifumo ya elimu kupitia maamuzi yanayosababisha kutengwa kimitaala, vitabu vinavyotumiwa na ubaguzi katika ugawaji wa rasilimali

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay amesema nchi 41 tu Ulimwenguni zinazotambua rasmi lugha ya ishara na kuwa shule nyingi zinang’ang’ana kuweza kupata intaneti kuliko kuwapa kipaumbele wanafunzi wenye ulemavu