Kwa mujibu wa tovuti yaa serikali, http://ngaradc.go.tz/
Asili /Chimbuko
Wilaya ya Ngara ni moja ya wilaya nane (08) za mkoa wa Kagera, Tanzania. Wenyeji wa Ngara ni Wahangaza na Washubi na wanaongea Kihangaza na Kishubi. Kabla ya kuitwa jina la Ngara, ilijulikana kama Kibimba yaani Pori. Chanzo hasa cha jina la Ngara ni sehemu iliyokuwa maalumu kwa mikutano, ambayo ilifanyika chini ya miti mikubwa inayoitwa iminyinya yingara. Hivyo, Mti wa umunyinya ulipandwa halmashauri ya wilaya ya Ngara kama kumbukumbu, kwani umebeba jina la wilaya ya Ngara. (Chanzo:Â https://www.jamiiforums.com/threads/historia-ya-wilaya-ya-ngara-utamaduni-wa-wakazi-wa-ngara-na-chanzo-cha-jina-la-kabila-la-wahangaza.1193348/).
Eneo
Wilaya ya Ngara ina ukubwa wa eneo lipatalo 3,744 Km2, imegawanyika katika tarafa nne (4) ambazo ni Nyamiaga, Kanazi, Rulenge na Murusagamba, kata 22, vijiji 75Â na vitongoji 389.
 Watu wa NgaraÂ
Wakazi wa wilayani Ngara wamegawanyika katika makabila mawili ambayo ni Wahangaza na Washubi. Kwa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2012 wilaya ina jumla ya kaya 63,293 zenye watu 320,056, ambapo kati ya hao 152,443 (47%) ni wanaume  na 167,613 (53%) ni wanawake. Ongezeko la watu kati ya sensa ya mwaka 2002 na sensa ya mwaka 2012 ni asilimia 2.7
Hali ya Hewa
Wilaya ya Ngara ina misimu miwili ya mvua, yaani mvua za vuli na za masika. Vuli huanza mwezi Septemba hadi Desemba na masika huanza mwezi Februari hadi Mei.  Kiwango cha mvua kwa mwaka hufikia wastani wa milimita 1400 kwa ukanda wa juu na milimita 800 kwa ukanda wa chini. Wastani wa joto kwa ukanda wa kusini ni 17 °C na ukanda wa kasikazini joto upanda hadi 25 °C.
Shughuli za Kiuchumi
Uchumi wa wilaya ya Ngara unategema shughuli za kilimo na ufugaji. Mazao makuu yanayolimwa ni kahawa, ndizi, mihogo, mahindi, maharage na mtama kwa upande wa mazao ya chakula. Mazao makuu ya biashara ni kahawa, ndizi na parachichi. Karibu asilimia 95 ya wakazi wa wilaya hii wanategemea kilimo kama chanzo cha mapato na shughuli za kilimo huchangia zaidi ya asilimia 94 ya pato la wilaya.
www.simamia.com imetembelea wilaya ya Ngara,ambayo kijiografia ipo kaskazini magharibi mwa Tanzania ikipakana kwa ukaribu sana na Nchi za Rwanda na Burundi. Â Baadhi ya Vijana wanazungumzia hatua ya Benki ya Dunia Kuiorodhesha Nchi ya Tanzania Katika Nchi za Uchumi wa kati kuwa hatua kubwa kimaendeleo huku kichocheo cha Uchumi ikiwa ni nguvukazi za vijana.
Ndaisaba George Ruhoro, ni mmoja wa vijana katika wilaya hii. Nimzaliwa wa Kijiji cha Karere Kata ya Kanazi ambaye amewaajiri vijana  walioajiriwa katika Kiwanda cha uchakataji,Usindikaji na Uzalishaji wa mafuta ya Alizeti.
Anaeleza kuwa, mawazo ya kuanzisha kiwanda hicho yalianza tangu mwaka 2010 licha ya kuwa Uzalishaji umeanza hivi karibuni mwakam 2020 lengo ikiwa ni kuwakwamua wakulima kiuchumi
Kupitia Kilimo cha Alizeti na uwepo wa Kiwanda hicho, Wananchi wa wilaya ya Ngara wanapata fedha katika sekta mbali mbali ambapo wakulima wanauza Alizeti kiwandani,huku vijana waliojiajiri kupitia Usafirishaji wa abiria na mizigo kwakutumia pikipiki maarufu kama Bodaboda pia wakiingiza kipato
Bwana Ndaisaba Ruhoro, anawahimiza vijana kufanya kazi kwa Bidii, kujiamini na zaidi kuzingatia sheria za Nchi, kanuni na maelekezo ya Serikali katika shughuli zao ili kuziidi kuipaisha Tanzania kiuchumi
Nuru Christopher Nzoya, Noela Temba na Erick Yunus ramadhani ni miongoni mwa vijana wanaonufaika kutokana na ajira kiwandani, ambao licha ya mafanikio ya Taifa kiuchumi,wanahamasisha vijana wenzao kujituma na kuzidisha jitihada katika kazi zao za Kila siku.
Baadhi ya wakulima za zao la Alizeti katika kijiji cha Mukarehe, Bw. Obadiah jonathjan na Ayoub Timothy wanajivunia uwepo wa kiwanda cha usikikaji wa mafuta ya Alizeti wilaya ya Ngara kama kichocheo cha maendeleo hasa wakati huu ambapo, Benki ya Dunia imeiorodhesha Tanzania katika orodha ya nchi za uchumi wa kipato cha kati.
I appreciate