Na
Mwandishi wetu
Uongozi ni kalama na kuna wengine wanasema uongozi ni majaaliwa ya Mungu ila sasa kuna uongozi wa kwenda kuusomea shule na kuteuliwa hawa wote ni viongozi waliopo nchini kwetu.
Kuna viongozi wa kuchaguliwa hawa ni kama Wajumbe,wenyeviti wa mitaa/vijiji na vitongoji,madiwani,wabunge na Rais.lakini pia kuna viongozi wa kuteuliwa hawa ni watendaji wa kata,watendaji wamitaa/vijiji,Wakurugenzi,wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa,mawaziri,makatibu nk.
Sasa hapa kila kiongozi anakazi yake kutokana na nafasi yake,aliyechaguliwa na wananchi huyu kazi yake ni kuwa kiungo msemaji na mpeleka kero kutoka kwa waliomtuma na kuwapa wenye mamlaka kwa muda huo.lakini pia kuna hawa walioteuliwa sasa hawa kazi yao ni kuwa kiungo wa boss wao wa juu kabisa yaani wapo kwa niaba ya rais.
Mfano Mkuu wa Wilaya yupo kwa niaba ya Rais na mkuu wa mkoa yupo kwa niaba ya Rais pia,kuna hwa mawaziri nao wanamuwakilisha rais pia sasa ishu ni kwenye ufanyaji kazi wao hapo sasa ndio tatizo linapooanzia.
Kuna baadhi ya viongozi wanajipa umungu mtu na wanataka wasujudiwe yaani kiufupi bila wao kutaka aiwi na wakitaka inakua hapo ndio tunasema hawa ni walevi wa madaraka na wanajishau kuwa cheo ni kama koti tu kabla hujawa nacho kuna aliyetoka ndio ukaingia ns wewe utaondoka atakuja mwingine.
Ukiingia baadhi ya ofisi za viongozi hasa huku chini huku kwa watendaji hawa wa kata na mitaa/vijiji unaweza ukazani ndio marais wa nchi yetu kunbe hamna ni watu tu ambao wamepeqa madaraka ya kuwahudumia wananchi ambao ndio maboss zao.
Hawa wanajisahau sana lazima tuwachane live maana huduma zao wengi wanatoa kwa kujisikia na wanapotaka,kingine wanatoa huduma kwa kukuangalia usomi na nafasi yako ikiwa msumbufu na unajua haki zako utaitwa mkorofi au mgeni tatizo hili yaani nakuaje mgeni kwenye nchi yangu?nikiwa ngara au dar bado nitaitwa NTZ.
Niwakumbushe viongozi acheni mazoea hayo ipo siku utatoka na kuacha hiyo nafasi atakaa mwingine saaa ukuwafanyia ubaya wananchi sijui huko uraiani utaishi vipi maana ukifanya ubaya jua ipo siku yatakukuta na wewe,mwaka 2023 umepita sqsa 2024 uwe mwaka mzuri na sio mwaka wa kujiona mungu mtu.
Recent Comments