WAKATI kukiwa na vita vya maneno kati ya Korea Kusini na Marekani, mikwara yao inayoambatana na tambo za matumizi makubwa ya silaha za nyukilia, inatikisa dunia ya wapenda amani.
Kiongozi kijana wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amekuwa akitoa vitisho vya kuishambulia Marekani, hasa katika kisiwa chake cha Guam, huku bilionea mtata, Rais Donald Trump, akisema endapo nchi hiyo inayoungwa mkono na China haitaacha vitisho vyake, itakiona cha moto.
Huku Korea Kaskazini ikifanya majaribio ya makombora yake ya masafa marefu yanayoweza kufika Guam, Marekani inasogeza manuwari zake za kivita, zinazoweza kuendesha mapambano katika rasi hiyo ya Korea, ikiwa na nia moja tu, ya kumshikisha adabu kijana huyo jeuri.
Kinachofanywa hivi sasa na wataalamu wa kijeshi wa Marekani ni kuangalia jinsi gani itakavyopunguza vifo vya raia wasio na hatia, sambamba na madhara mengine ya kibinadamu, mara tu âshughuliâ ya kuiangamiza nchi hiyo itakapoanza.
Japan, ambayo nayo huenda itashambuliwa na Korea endapo vita hivyo vitapiganwa, inaiomba China, mshirika wa karibu wa Kim, kutumia ushawishi wake kuepusha mapigano, kwani kwa namna hali inavyokwenda, âhaitamuacha mtu salamaâ.
Mkurugenzi wa zamani wa Mawasiliano katika Ikulu ya Marekani, Anthony Scaramucci, amesema ingawa bosi wake huyo wa zamani anataka suala hilo limalizike kwa njia ya mazungumzo, lakini pia anayo plan B, yenye nia ya kuiadhibu vilivyo Korea Kaskazini.
âNadhani Marekani ina suluhisho la jambo hilo, suluhisho la kwanza ambalo mara zote ndilo hutangulia, ni mazungumzo ya kidiplomasia na kama hilo litashindikana, basi Donald Trump ana utatuzi mwingine kama itamlazimu,â alisema.
Recent Comments