Na
mwandishi wetu
Wilaya ya ngara ni miongoni mwa wilayani zilizobarikiwa nchini Tanzania kuwa na hadhi ya mipaka na nchi jirani(Boda ya Tanzania na Burundi(Kobero)na boda ya Tanzania na Rwanda(rusumo).
Vilevile ngara imebarikiwa kuwa na madini aina ya Nickel ambayo madini hayo kwa sasa bado hayajaanza kuchinjwa ila mchakato wa kuhamisha watu unaendelea,Madini hayo yanaweza kuzalisha Betri za magari na vifaa vingine.
Jambo la kumshukuru Mungu kwa ngara ni kutokana na kubarikiwa ardhi nzuri na kubwa kwa kilimo,huku wananchi wakilima mazao ya chakula na biashara kama maharage,mahindi,Parachichi,kahawa hata ndizi.
Cha ajabu na chakusikitisha Wilaya ya ngara hivi karibuni kumetokea shida ya upatikanaji wa mafuta ya petrol kwa watumiaji vyombo vya moto kama gari na pikipiki. Awali shida hii ilipotokea simamia.com ilifanya uchunguzi na kugundua mafuta yapo kwenye vituo isipokuwa walikua wanauza kwenye madumu na kujificha(kwa gharama kubwa hasa kwa warundi).
Hapo bei ya petrol ilikua 2940+ na ikaonekana sehemu kubwa ya wamiliki wa vituo vya mafuta wakilalamika bei ndogo na wanaoata hasara,hapo ndipo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikaliona tatizo na kuanzia mwezi wa 9 bei ilipanda kwa ngara mpaka ikafikia 3400 kwa lita moja ya petrol.
Sasa basi watumiaji wakajua ehee hapa tabu imeisha na ni kweli kwa muda mfupi watu waliinjoy ila baada ya muda mambo yamerudi palepale baadhi ya vituo vya kujazia mafuta wanafunga vituo na wengine wanaweka na uzio kabisa kuonyesha hawataki watu wanunue au wasogelee kabisa.
Ok ishu ingekua mafuta hamna basi watu wangeelewa ila shida ni kwamba mafuta yapo baadhi ya vituo na hawawajazii watu labda uende kwa kujiiba na wanakuuzia dumu la lita 20 elfu 80 jambo ambalo ni tofauti na bei iliyopangwa.
Swali la kujiuliza hivi hii hali serikali ya wilaya inalijua na je kama inalijua imechukua hatua gani?kama pia hawalijui kwa nini ?maana hata baadhi ya viongozi na polisi wanapeleka magari yao wanajazia tena mchana kweupe watu wanaona ila raia hufunguliwi sasa hii imekaaje?
Baadhi ya wananchi hasa wa kabanga wameomba habari hii itolewe na iwafikie viongozi ngazi ya mkoa hata waziri husika ili kuwasaidia maana kiukweli watu wengi wamenunua magari na pikipiki nyingi lakini changamoto ni mafuta na namna wanavyofanyia.
Ikiwa ni mwisho wa makala simamia.com ilizunguka na kukuta watu wakiuza mafuta kwenye chupa za lita moja na nusu kwa 7000 mpaka 8000,swali la kujiuliza kama vituo havina mafuta hawa wachuuzaji wanayapata wapi?na je uchumi wetu unaenda wapi?na je hawa wanaouza mafuta bei ya juu tena kinyemela kodi wanalipa wapi?
Recent Comments