Wachimbaji wawili wa madini ya dhahabu katika machimbo ya Mwime yaliyopo katika halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wamefariki dunia baada ya kuangukiwa kifusi cha udongo wakati wakiwa wanachimba madini ndani ya duara.
Taarifa iliyotolewa leo na kamanda wa polisi mkoani humo (ACP) Debora Magiligimba imesema kuwa tukio hilo limetokea febuari 12 mwaka huu majira ya saa mmoja asubuhi katika duara namba 11C wakati wakiwa katika harakati za kuchimba madini ya dhahabu.
Kamanda Magiligimba aliwataja walifariki dunia ni pamoja na Kija Walaga( 25) mkazi wa Mwime na Msonga giti ( 36) mkazi wa Itilima, mkoani Simiyu na kusema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kufanya shughuli za uchimbaji bila ya kuzingatia tahadhari kutokana na duara hilo kutotumika kwa muda mrefu.
âNitoe rai kwa wachimbaji wote kuzingatia tahadhari pindi wanapotekeleza majukumu yao hususani katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha,duara hilo lilikuwa limefungwa kwa lengo la kufanyiwa matengenezo na kama wangezingatia taratibu za kiusalama kusingetokea kwa vifo hivi,âalisema Magiligimba.
Sambamba na hilo Kamanda Magiligimba amezikumbusha kamati za usimamizi wa madini kuhakikisha zinasimamia miongozo ya usalama mahala pa kazi ili kuepukana na ajali zisizokuwa za lazima ambazo zinachangia kupunguza nguvu kazi ya taifa.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya halmashauri ya manispaa ya Kahama ikisubiri taratibu za mazishi.
Recent Comments