Recent Comments

WAKULIMA WA KAHAWA NGARA WAPOTEZA NURU.

By Mwafrika Feb 10, 2024

NA,ANKO G

Wakulima wa zao la Kahawa wilayani Ngara wamepoteza Nuru baada ya kumpoteza alie kuwa meneja wa Ngara farmers Bw. Zephania Edward Mnyonyera kwa ajali ya gari.

Aidha Bw.Mnyonyera amekua kiongozi mwenye maono makubwa ya kupaisha soko la zao la kahawa ndani na nje ya nchi ya Tanzania hasa Korea na Japan kipindi cha uhai wake.

Hata hivyo kumpoteza kiongozi huyo ni pigo kubwa kwa wakulima wa zao la Kahawa wilayani Ngara.

Uongozi na wafanyakazi wa simamia.com tunatoa pole kwa familia ya Mnyonyera na wakulima wote wa Kahawa wilayani Ngara.

Ayu 1:21 SUV
akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.

Kwa taarifa zaidi endelea kutembea simamia.com.