Chama cha walimu wilaya ya Kasulu mkoa wa Kigoma (CWT) kimewataka walimu
kuepuka kubadili changamoto zao kuwa adhabu kwa wanafunzi madarasani.
Hayo yalisemwa na katibu wa chama hicho wilaya ya kasulu mwalimu Cassian
Kosta Mbajije wakati akizungumza na Mwandishi wetu kwenye ofisi za CWT
wilayani humo juu ya mkakati na mchango wa chama cha walimu kwenye
kuongeza ufaulu kwa madarasa ya mitihani.
Mwalimu mbajije alisema kuwa changamoto za walimu zipo nyingi hata sio
Kasulu tu yaweza kuwa za nchi nzima lakini matokeo mazuri kwa wanafunzi yafaa
kuwa kipaumbele cha kwanza kabla ya kuiwaza fedha .
âchangamoto zao zisihusishwe na wanafunzi badala yake watimize wajibu wao
wa kutoa maarifa wakati chama kikiendelea kuisukuma serikali kutatua
changamoto walizanazo walimu âalisema Mbajije
Kuhusu ushirikiano wa CWT na halmashauri katika kuboresha kiwango cha ufaulu
alisema kuwa wamejiwekea utaratibu wa kuwapatia mafuta ya pikipiki waratibu
elimu ngazi ya kata ili waweze kufanya ufuatiliaji bila visingizio vya kushindwa
kufika kwenye shule.
âkasulu inazo halmashauri mbili, kwa halmashhauri ya kasulu mji baada ya vikao
vya wadau tulikusudia kupandisha ufaulu kutoka asilimia70-74 hii ni kwa shule za
msingi na sekondari iwe 80-90, na upande wa halmashauri ya wilaya tulikusudia
shule zamsingi tutoke asilimia 73-80 na sekondari iwe asilimia 90-94 na lazima
tufanikwe kwakuwa tulikusudia kufanya kazi kwa pamojaâ. alisema Mbajije
Aliongeza kuwa mpango wa kuwapatia waratibu elimu kata mafuta ya pikipiki
ulianzia katika halmashauri ya wilaya kwa kuwapatia mafuta waratibu wote wa
kata 15 na Kwamba utaratibu kwaajili ya kasulu mji yenye kata 21 nao upo katika
hatua za mwisho ili nao wapate mafuta ya pikipiki.
MWISHO.
Recent Comments