Recent Comments

WANANCHI 300 NGARA WALALAMIKIA KUTO LIPWA FIDIA ZA MRADI WA UMEME RUSUMO.

By Mwafrika Sep 16, 2023
Baadhi ya nyumba za wananchi wanaoishi eneo la tukio

WANANCHI 300 NGARA WALALAMIKIA KUTO LIPWA FIDIA ZA MRADI WA UMEME RUSUMO.

NA, MWANDISHI WETU

Wakazi wasio pungua 300 wa kata ya Ntobeye na Kirushya walalamika kutolipwa fidia baada ya kuathiriwa na maji katika mashamba yao na makazi yao kati ya mwaka 2018 na 2020.

Vilevile simamia.com imefika katika kata hizo ambapo Ndg.Abel Rauben Kazuzi mkazi wa kijiji cha Chivu na Mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji wa wakazi walio athiriwa na mradi huo amesema kuwa mradi huo uliathiri Kijiji cha Chivu,Runzenze,Kirushya na Kasange ambapo tathimini yakwanza ilifanyika mwaka 2011 ambapo ziliwekwa alama nyeupe ambapo maji yataathiri ambapo tathimini ya mwaka 2012 ilifanyika tathimi nyingine kwa kusogeza vingingi na kuweka alama nyekundu.

Ndugu Abel kazuzi(Mwenyekiti kamati ya ufuatiliaji)

Hata hivyo baada ya hapo ilifanyika tathimini na kutoa karatasi za kuwatambua watakao athiriwa na maji ambazo zingetumika kuwalipa fidia.

Baadhi ya karatasi walizopewa baada ya mchakati wa kutathmini

Hata hivyo maji yaliathiri maeneo hayo kati ya mwaka 2018 na mwaka 2020 ambapo kufikia mwaka 2021 Diwani wa kata ya Ntobeye Bw. Sanday Mkozi alifika ofisi ya Mkuu wa wilaya Kanali Mathias Kahabi baada ya hapo wakafika NELSAP katika eneo hilo pamoja na afisa ugani Bw.Kabebo na kualika wanachi ndipo NELSAP wakaagiza kuunda kamati ya ufuatiliaji yenye wajumbe nane (8) ambapo kamati hiyo imekua ikifuatilia suala Hilo bila kupata matunda mpaka hivi sasa.

Hivyo basi kamati hiyo kwa kushirikiana na wanachi hao hao wanatazamia kufikisha malalamiko yao kwenye ofisi ya Wazuri mkuu kwani tayari analifahamu na tayari aliwahi kulitolea maelekezo kipindi alipo fika katika wilaya ya Ngara.

Baadhi ya nyumba za wananchi wanaoishi eneo la tukio
Pia baadhi ya wanachi ambao wameathiriwa na mradi huo hawana tena maeneo ya kulima wamashindwa kujikimu kimaisha na kujenga nyumba nzuri badala yake wanaishi katika nyumba za majani ambazo siyo imara hasa kipindi hiki cha mvua.