WANANCHI WA KATA YA CHOME WILAYANI SAME WAPEWA ONYO KILIMO CHA MIRUNGI.
Na Musa Mathias Njogolo.
Email. mussamathias573@gmail.com musamathiasnjogolo@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni amewaonya wananchi wanaoendelea na kilimo cha madawa ya kulevya aina ya Mirungi na kuwataka kuacha mara moja kutokana na athari kubwa zinazoweza kujitokeza huku akitangaza Oparesheni maalumu ya kuwasaka watakao kaidi agizo hilo.
Mhe. Kasilda ametoa onyo hiyo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliolengaa kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi wa Kata ya Chome ambapo amesema kuwa zao hilo limekuwa likiathiri nguvu kazi ya Taifa.
“Kati ya tarafa ambayo inaongoza kwa ulimaji wa Mirungi ni tarafa ya Chome Suji Mirungi ni madawa ya kulevya na yanaathari kubwa kwa binadamu ikiwemo ukatili na kujichukulia sheria mkononi lakini haya madawa yanaathiri akili sana”
Aidha mkuu wa wilaya huyo amewashauri wananchi hao kulima mazao mbadala ya biashara ikiwemo parachichi kutokana na hali ya hewa ya milimani inaonesha kuwa kilimo hicho kinastawi kwa kiwango kikubwa na hivyo jamii itanufaika sana kwa kuongeza kipatoq na kuwa salama.
Pia amewaonya viongozi wa vijiji na vitongoji ambao wanaodaiwa kuhusika na kilimo hicho kuacha haraka iwezekanavyo Serikali inahitaji viongozi waadirifu wanaotatua kero za wananchi na kusimamia maendeleo ya maeneo yao.
Aidha amewataka wananchi kuanza kufanya upembuzi wa viongozi wa serikali za mitaa wakati tunaelekea kwenye uchaguzi ambao hawastahili kutokana na baadhi yao kujihusisha na kilimo cha mirungi hivyo wananchi hao wametakiwa kuangalia viongozi wanaofuata maadili ya uongozi.
Mwisho.
Recent Comments